Ticker

6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA PROF.IDD MKILAHA ATOA TAHADHARI

Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania imetoa taadhari kwa wananchi wanaotumia vyakula vinavyotoka nje ya nchi kuhakikisha wanakula vyakula ambavyo vimepimwa na kukaguliwa na tume hiyo ili kuweza kuhakikisha havina chechembe za mionzi ambayo ilisababishwa na kulipuka kwa vinu vya Nyuklia vilivyopo katika mji wa Fukushima nchini Japan.



Akiongea na waandishi wa habari mjini hapa mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Iddi Mkilaha alisema kuwa wameamua kutoa taathari hiyo kutokana na milipuko ya vyungu vya Nyuklia uliotokea ambapo wameona ni bora watoe taathari mapema ili usiweze kuleta mathara hapa nchini .



Alisema kuwa kutokana na umbali kati ya Tanzania na Japan kwa kiasi cha mionzi kilichochafua hali ya hewa ya eneo hili na mfumo wa upepo duniani kunauwezekano mdogo kwa chembechembe za mionzi kufika nchini kwa njia ya anga.



Aidha alisema kuwa tume inapenda kutahadharisha kuwa upo uwezekano wa chembechembe za mionzi zilizochafua mazingira kuweza kuchafua baadhi ya bidhaa hasa za vyakula kutoka eneo la tukio na pengine hata katika nchi jirani ya eneo la tukio napengine kuingizwa hapa nchini na kuleta mathara.



Mkilaha alisema kuwa hivyo kufuatia mamlaka iliyopewa kisheriana kanuni husika (Atomic Energy Act and Regulation)tume hiyo imejipanga kuongeza nguvu ili kuhakikisha kuwa bidhaa zote za vyakula zinazoingizwa nchini zinakaguliwa na kuhakikiwa na kupewa kibali hazitakuwa na chembechembe za mionzi .



“kutokana na hali hii hivyo tume hii ambayo imepewa thamana la kuhakiki kuwa bidhaa zote za vyakula vinavyoingia kutoka nje ya nchi hazina chembechembe hizi za mionzi hiyo ambayo ikiwa bidhaa zitaingizwa zikiwa nazo zinaweza kuleta madhara kwa watanzania watakao tumia”alisema Mkilaha



Alisema kuwa mionzi hii inamathara makubwa kwa binadamu ambayo yanaweza kuwepo ya mda mrefu na hata mfupi hivyo ambayo huweza kusababisha magonjwa ya saratani hivyo watajitaidi kuweka nguvu kubwa ili kudhibiti hali hiyo isiingie hapa nchini.



Alibanisha kuwa tume pia imeamua pia tume hii inaendesha kituo cha upimaji mionzi katika anga kilichopo Dar es salaam chenye uwezo wa kugundua chembe chembe za mionzi zinazoweza kutufikia iwapo kutakuwa na tukio lenye kuchafua hali ya hewa kwa mionzi.



Alisema kuwa pia katika kipindi hiki tume hiyo itaendelea kuiarifu serikali kupiita wizara ya mawasiliano sanyansi na teknolojia juu ya tukio hilo na matukio yote yanayohusu athari za mionzi na itaendelea kuwaarifu wananchi iwapo kutakuwa na uwezekano wowote wa ahari za mionzi.



Mionzi hii ambayo taathari yake inatolewa ilitokana na tetemeko kubwa la ardhi nchini ya bahari lilosababisha mawimbi makubwa ya bahari (tsunami) lililotokea huko kaskazini mwa japani mapema marchi 11mwaka huu ambapo vinu vya kituo cha uzalishaji wa umeme wa nuklia vulivyoko katika mji wa fukushima kilipata uharibifu mkubwa uliosababisha mfumo wke wa kupooza mitambo kuharibika na hatimaye kuleta milipuko.

Post a Comment

0 Comments