Taasisi ya Kimataifa itakayorithi kazi zitakazoachwa na Mahakama ya
Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) mjini
Arusha,Tanzania,itaanza kazi rasmi Jumatatu ijayo.
Miongoni mwa kazi za taasisi hiyo ijulikanayo kwa kifupikama IRM
ni pamoja na kuendelea kuwasaka watuhumiwa watatu maarufu ambao bado
hawajatiwa mbaroni, akiwemo mtu anayesadikiwa kuwa ndiye mfadhili wa
mauaji hayo,Felicien Kabuga.
Kabuga anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya kimbari ikiwa ni pamoja
na madai kwamba alinunua mapanga ambayo yanadaiwa kutumika kwa kiasa
kikubwa katika mauaji dhidi ya Watutsi wakati wa mauaji hayo mwaka
1994.Mshitakiwa huyo ni ndugu yake aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal
Habyarimana.
Washitakiwa wengine wawili waliobaki ni pamoja na Waziri wa Ulinzi wa
zamani waRwanda, Augustin Bizimana na aliyekuwa Kamanda wa Walinzi wa
Kikosi cha Rais, Protais Mpiranya.
Naye Mwendesha Mashitaka wa ICTR, Hassan Bubacar Jallow Julai 2, 2012
pia atakuwa Mwendesha Mashitaka wa IRM. Alikuwa kila mara akitoa wito
kwamba ‘’vigogo’’ hao washitakiwe na mahakama ya kimataifa. ICTR
imeshasikiliza ushahidi maalum kuhusu watu hao watatu ambao bado
wanatafutwa ili ushahidi huo uweze kutumika hapo baadaye iwapo watatiwa
mbaroni.
‘’Kuwasaka washitakiwa vigogo hao watatu kutaendelea kuwa changamoto
huku zikiwepo taarifa zinazomhusisha Kabuga kuwa yuko nchiniKenya,
Mpiranya yukoZimbabwena Bizimana anatajwa kuwa yupo katika maeneo
mbalimbali ya kanda hiyo pia,’’ Jallow alisema katika hotuba yake
aliyoitoa Juni 7, mbele ya Umoja wa Mataifa (UN).’’ Ni muhimu kwa
kuzingatia suala la amani na haki, nchi zote ziunge mkono juhudi za ICTR
katika kuwasaka watuhumiwa hao,’’ alisema.
Baadhi ya vyanzo vya habari vinadai kwamba Bizimana na Mpiranya
wamekufa lakini Ofisi ya Mwendesha Mashitaka inakana. Kwa mujibu wa
mwendesha mashitaka madaikamahayo ni ujanja wa kuwasaidia watu hao
kukwepa mkondo wa sheria.
Wapo watuhumiwa wengine sita wa ICTR
wa ngazi ya chini ambao pia bado wanasakwa. Mahakama hiyo ya Umoja wa
Mataifa pia imeanza kuhamisha majalada ya kesi nyingine za watuhumiwa
kwenda kusikilizwa nchini Rwanda kama sehemu ya mkakati wa kuhitimisha
kazi za mahakama hiyo.Kazi ya kuwasaka watuhumiwa sita hao sasa itakuwa
chini ya Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu nchini Rwanda.Watu hao sita
wanajumuisha Luteni Kanali mmoja, mameya wa zamani watatu, inspekta wa
zamani wa polisi na mmiliki wa mgahawa.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia