mwanachama mma mjane akipokea kadi ya uwanachama wa CUF katika mkutano uliofanyika jijini Arusha
KAti kati ni aliyekuwa diwani wa kata ya elerae John Bayo ambapo alirudisha kadi ya chadema na kurudi katika chama chake cha awali CUF
CHAMA cha wananchi (CuF) jana kimeuteka mji wa Arusha baada ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa Levolosi jijini hapa na kuwataka wakazi Arusha kutowachagua viongozi wanaowapatia vijana pombe za viroba na konyagi kwa lengo la kufanya vurugu.
Katika
mkutano huo diwani wa kata ya Elerai aliyefukuzwa ndani ya Chadema,John Bayo
alijiunga rasmi na chama hicho huku akitaja sababu iliyomfaya ajiunge ni baada
ya kuona chama hicho kinaendeshwa kwa rimoti na mbunge wa amani wa jinmbo la Arusha mjini,Godbless
Lema.
Akihutubia
umati wa watu waliofurika katika viwanja hivyo,mwenyekiti wa Cuf taifa,Prof
Ibrahim Lipumba aliwataka wakazi wa Arushakutowapa fursa baadhi ya viongozi wa
kisiasa mkoani Arusha mabo wamekuwa wakihamasisha vurugu na mauaji.
Biala kutaja
majina yao hadharani Lipumba alisema kwamba baadhi ya viongozi wa kisiasa
mkoani Arusha wameshindwa kusimamia
maaadili ya uongozi na badala yake wamekuwa wakiwapa pombe za viroba na konyagi
vijana ili wafanye vurugu.
“Wengine
wanawapa vijana viroba na konyagi wafanye vurugu tunahitaji viongozi wenye
kuisimamia Arusha sio wanaowapa viroba
wafanye vurugu”alisema Lipumba huku akishangiliwa na wafuasi wa Cuf
Hatahivyo,aliusifia
mji wa Arusha kwamba ni mji wa kitalii duniani na inachangia pato kubwa kla
taifa lakini amani ndiyo imekuwa ikitia doa katika uso wa dunia.
Alisema
kwamba rasilimali za taifa kama madini ya Tanzanite yaliyopo Mererani mkoani
Manyra yamekuwa hayatumiki ipasavyo pamoja na kutajirisha nchi nyingine huku akisema
kwamba ni lazima wapatikane viongozi wa kusimamia rasimali hizo.
Hatahivyo,aliponda
sera ya majimbo inayotamkwa na Chadema huku akisema kwamba sera hiyoitachagia
mpasuko kwa taifa na kudai wao sera yao ni kuwaunganisha watanzania bila kuwabagua
wanakotoka.
Naye,katibu
mkuu wa chama hicho ambaye ni makkamu wa kwanza wa Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharif
Hamad akihutubia viwanjani hapo alilaani baadhi ya vyama vya siasa na wanasiasa
kutumia nguvu kazi ya vijana vibaya kwa kuwapa pombe za viroba badala ya
kuwajenga kiuchumi.
Alitoa rai
kwa wanasiasa nchini na mkoani Arusha kufanya siasa za kistaarabu kwa kuwa
amani iliyopo kwa sasa pindi ikitoweka itawagharimu watanzania kuirudisha na
watahukumiwa na damu iliyomwagika ardhini.
Naye,naibu katibu mkuu wa chama hicho upande
wa bara,Julius Mtatiro aliutumia mkutano huo kumshambulia aliyekuwa mbunge wa
jimbo la Arusha mjini,Godbless Leman a kumtaka aache kuwatumia vijana wa
Arusha kufanya vurugu na badala yake awasaidie kimaendeleo.
Mtatiro,alipinga
madai ya udini ambayo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiinyoshea Cuf na kusema
kwamba kule alikozaliwa mkoani Mara waislamu na wakristio wanaishi kwa amani
kama ndugu na kudai chama chao kina madiwani katika wilaya za mkoani humo ambao
ni waislamu na wanashirikiana bila ubaguzi na wa dini nyingine.
Katika hatua
nyingine chama hicho kilitangaza kuweka kambi mkoani Arusha hadi kieleweke kwa
lengo la kukieneza chama hicho huku kikisema kwamba uwekaji wa kambi Arusha
utakifanya kiifikie mikoa ya Klimanjaro,Tanga na Manyara kwa urahisi.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia