Ticker

6/recent/ticker-posts

MAPENZI SHUBIRI YANATOA ROHO YA MAMA FATU.FUHATILIA HADIDHI HII ILIANDIKWA NA MWANDISHI MASHUHURI WA VITABU



NDUGU YANGU MWENYE KUPENDA,CHONGO HUONA KENGEZA/MAMA FATU AKATESWA KULE SINZA,AKAZUNGUKA NA MJI HUKU AKITOKWA MACHOZI,AKIKONDA,AKIDHANI DUNIA IMEMPA KISOGO NA SIYO YAKE BALI YA WENZAKE.NAKUTANA NA MAMA FATU USO KWA USO PALE MWENGE DAR ES SALAAM,ANANIKIMBILIA NA KUNIKUMBATIA,ANAONEKANA KAMA NI MTU ASIYEAMANI KAMA TUMEONANA,ANALIA KWA FURAHA YA KUONANA NAMI.PIA NAMSHIKILIA VYEMA NGUO ALIZOVAA ZISIMDONDOKE KWANI ALIKUWA KAMA AMEINGIWA `MAJUNUNI`.NAMSIHI ANIACHIE KWA MUDA HUO KISHA TUSABAHIANE,,ANAZIDI KULIA..WAJA WAPITA NJIA WANATUTAZAMA KWA MACHO TELE..NAMSHIKA MAMA FATU MIKONO NA KUMPELEKA KATIKA HOTELI MOJA ILIYOPO JIRANI,ANAAGIZA SODA YA BARADI.ANAZIDI KULIA NA KUTETEMEKA.DHAHIR ALIONEKANA ANAHITAJI MSAADA WA MAWAZO HARAKA..UMRI WAKE NA WAKE NI VITU VIWILI TOFAUTI LAIKINI ALIAMINI NAWEZA KUMSAIDIA NA KUMNASUA KATIKA TOPE ZITO LA MAHABA BATILI YANAYOELEKEA KUMTOA UHAI..AMEPIGWA NA MAPENZI.NAMTAZAMA KATIKA MBONI YA MACHO YAKE,NAONA WEKUNDU NA MACHOZI YANAMWAIKA..MDOMO UNAMTETEMEKA..SODA ALOAGIZA BADO HAJAWEKA KINYWANI..NATOA KITAMBAA NA KUMFUTA MACHOZI,,HUKU NIKIMSIHI AWE MVUMILIVU NA KUNIJUZA `KULIKONI`.MWILI NILOMKUTA NAO MAMA FATU SI WAKWAKE..MACHO YAKE MALEGEVU YAPO PALEPALE.ANATAMKA NENO MOJA ``NDOA` NA KUANZA KULIA TENA..ANAJIVUTA NA KUVUTA PUMZI NDEFU KISHA ANATAMKA NENO LA PILI ``MAPENZI``KISHA ANALIA TENA KWA SAUTI KUU ..NAPATA TASWIRA KUWA TAYARI KESHAPIGWA NA MAPENZI NDANI YA NDOA..NAVUTA KUMBUKUMBU NAMUONA MAMA FATU MWENYE UMBO KUBWA NA ZURI MIAKA SABA ILIYOPITA KULE ARUSHA..NAMUONA MAMA FATU AKIWA NA TABASAMU PANA ULIYOAMBATANA NA MWANYA,NAONA USO WAKE WA JAMALA,,SAUTI YAKE YA `KIBARAWA` MITHILI YA MWIMBAJI MALIKA KULE MOMBASA.MACHO YAKE MAKUBWA YALOZUNGUKWA NA WEUSI MITHILI YA MWIMBAJI WA TAARAB BI.MWANAHELA KULE TANGA..NAZIDI KUONA SURA YA MAMA FATU YA MIAKA 7 ILIYOPITA NA KUINAMISHA KICHWA CHINI ( SUBB-HANNAH-LAAH)…HAIBA IMEPOTEA UZURI UMEMTOKA,MALI IMEANGAMIA MARADHI HAYAKUMTOKA,MSIPENDE UGENINI MTAINGIA HATIANI,KUPENDA KITU ADHIMU NAWAMBIA KUNA DAWA..MSIKILIZE MAMA FATU KISHA TUMSAIDIE…  
KIla nikiwaangalia wanangu Fatu  na abdi nashindwa namna ya kudai talaka kutoka kwa mume wangu Rama.Watoto wangu wakilelewa na mwanamke mwingine sidhani kama watapata haki zao na hata kusoma hawatosoma.
 
Kama tabu ni mauti leo mimi faudhia`mama fatu `nisingalikuwepo.Kucha kutwa mume wangu anashinda baa,mshahara akipata ndiyo nyumba anaihama kabisa.Siku moja mchana wa ijumaa nilikaa sebleni na radio yangu nikiskiliza.hewani  mtangazaji aliweka nyimbo ya marehemu Marijani Rajabu na nyimbo yenyewe iliitwa ukewenza,..niliskiliza mashairi ya ule wimbo ,,hakika yaliniingia na nikaanza nami kuimba kwakuifuatisha...unitizame ..nilivyokondaaa,,sababu ya ukewenzaa...ukewenza mimi sitaki jama sitaki mamaa,,,,)
 
Punde nyimbo hiyo ikiwa hewani akaingia Baba fatu.Hapo ni baada ya kutokuonekana kwa siku kumi akidai gari kubwa analoendesha kwenda mikoani kuharibikia chalinze akiwa anarudi akitokea Arusha.Nilimpa pole naye akaitikia asante.Aliomba maji ya kunywa nikampatia.alivyomaliza maji akaniuliza habari za watoto nami nikamjibu kuwa hawajambo,akauliza wako wapi sasa? Nikamjibu Fatu yupo shule na Abdi ameenda katika mizunguko yake huko kupiga piga `debe`..
 
Hakika kama kuna jambo ambalo sitolisahau ni hili la mimi kumpenda mume wangu kupita kiasi.
nadhani pia upendo wangu kwake ndiyo uliyosababisha mimi kuteseka kiasi hiki.Nilimwekea maji ya kuoga akaenda kuoga aliporudi tukakaa mezani nikatenga chakula kisha tukaanza kula.
 
Tukiwa mezani kwa mbali niliweka taarab asilia,mwimbaji alikuwa ni bi shakila saidi,nyimbo iliitwa mapenzi yamepungua ```mapenzi yamepunguaa,,mimi nimeshayaona..kila nikiyaachunguaa,,hatwishii kuoneanaaa..mapenzi  yamepunguaaa) Niliweka kanda ile kwa sababu maalum) kwakuwa mume wangu alibadilika,mapenzi yake kwangu yalishaanza kupungua,,nilianza kupata shaka.Yeye nadhani hakuelewa ni kwanini nimeiweka nyimbo ile ambayo niliipenda sana.Wakati tunakula simu yake iliita,,aliangalia kisha akaichukua na kuingia chumbani.Alimaliza kuongea na simu hiyo kisha akarejea na kuendelea kula.Sikumuuliza chochote.Baada ya wiki  mbili,mume wangu alirejea akanambia amefukuzwa kazi kwasababu gari alilokuwa akiendesha limeibiwa baadhi ya vifaa alipokuwa amelipaki na boss wake amemwachisha kazi kwasababu ya uzembe.
 
Hakika niliumia sana tena pengine kuliko hata mume wangu.Niliwaza mimi sina kibarua ni mama wa nyumbani,tuna watoto wanasoma,nyumba niya kupanga,tutaishi vipi yailahh kwakuwa hata wakati akiwa na kazi bado maisha yalikuwa ni magumu na tulikuwa tukilala na njaa wakati mwingine.
 
Nililia sana ila sikusahau kusali na kumuombea mume wangu apate kazi nyingine.Mimi nilikuwa nikicheza `kibati` na akina mama wenzangu ,nilipopokea shilingi milioni moja niliacha kucheza ili nijue nitaitunza vipi familia yangu na mume wangu mpaka atakapopata kazi .
 
Nilipopata ile fedha nikaanza kuuza vitumbua na chapati nje ya nyumba yetu.Maisha yaliendelea huku mume wangu akiendelea kutafuta kazi nyingine bila mafanikio.
 
AKirudi katika mizunguko yake anakuta chakula na watoto wanafuraha kama kawaida,nilihakikisha najibana na kuzalisha fedha izo ili tuweze kuishi.Siku moja nikiwa napika chapati nje ya baraza letu alikuja mtu mmoja wa makamo akiwa na gari aina ya Suzuki vitara,alisimamisha gari lake na kunambia nimletee chapati tano nilimfungia na kumpelekea,akanipa fedha zangu,nikiwa narudi akanipigia honi,nilipogeuka akaniita tena,nikaenda,akaanza kuniuliza naitwa nani,nikamwambia naitwa mama fatu,akanambia nimpe jila langu kamili nikamwambia naitwa Faudhia,akasema anashkuru kunifahamu nayeye akanambia anaitwa Hamza,nami nikamwambia nashukuru kumfahamu mteja wangu mzuri wa chapati.
 
Akanambia anaomba namba zangu za simu,,nikamwangalia kisha nikaguna.mmh.nikamuuliza za nini jamani wakati kila ukija hapa kununua chapati unanikuta mimi? Akanijibu kuwa anaomba tu namba za simu kwakuwa kuna jambo jingine anataka kunambia kwa njia ya simu.Nikamwambia mimi nimeolewa na mume wangu huwa anafuatilia sana simu yangu..akanambia nisiwe na shaka kwakuwa anafahamu kama nina mume hivyo atatumia vizuri namba zangu..nilimpatia namba zangu.Aliendelea kupita mara kwa mara na kuja kununua chapati asubuhi huku akinisabahi na kupita.Wakati huo nilikuwa na jukumu kubwa la kuitunza familia yangu na mume wangu pia nilibeba jukumu la kumtunza.Siku moja mchana Hamza alinipigia simu akaniomba jumapili tuonane mjini.Nikamuuliza kuna nini ,akasema anaomba sana nisimwangushe tukutane mjini kuna suala muhimu anataka kuongea nami.Nikamwambia aongee katika simu nitamwelewa.akakataa ,nami nikakataa kumfuata mjini.
 
Alikata simu lakini baada ya dakika tatu alipiga tena,akanambia mbona mimi nakuwa kama siyo mtu mzima simwelewi? Nimkamwambia aseme tu nitamwelewa,,akasema amenipenda sana yupo tayari kufanya lolote anipate hata ikibidi kuishi pamoja kwakuwa yeye bado hajaoa.
 
 Nikamwambia anisamehe sana mimi nimeshaolewa na ninampenda sana mume wangu sipo tayari kumsaliti licha ya kuachana naye.`kwakweli nampenda sana mume wangu ni kifo tu ndiyo kitatutenganisha wala sitomwacha nilimkatia simu na kuingia chumbani kwangu,alipiga simu tena nikakata.Nilitafuta kanda za mwanamuziki marijani rajabu nikaanza kusikiliza ili kuondoa mawazo kwakuwa nilimpenda sana marehemu marijani rajabu..
 
niliweka nyimbo ya `mpenzi Aisha`Nilianza kuimba nikimfuatisha Marijani kama kawaida yangu..``Sikiliza tamkoo..sikiliza kwa makini,,tamko la moyoni,,ama kweli pendo lako limeingia moyoni mwanguu,,`Hakika mashairi ya marijani huwa nayanipa hamasa sana..nilihamasika na kufunga macho na kuona sura ya mume wangu mpendwa.Nilianza kukunja nguo nilizofua jana . Jioni ilifika na mume wangu alirejea na baada ya kuoga tulikaa mezan.Cha ajabu na kilichonistaajabisha ni kitendo cha mume wangu kulewa siku hiyo,nilimuuliza kwanini umelewa na maisha yenyewe ndiyo haya? Akanijibu kwa sauti ya kilevi...``aah nakunywa kuondoa mawazo kazi yenyewe ngumu kupatikana`.Niliangalia chini na nikaingia chumbani kwangu nikamwacha anakula na watoto..Nilitoa radio yangu na kuweka kanda ya muziki wa zamani alikuwa ni Marijani Rajabu nyimbo iliitwa `pombe siyo chai`.Tulipoingia ndani wakati wa kulala nilimsihi mume wangu aache pombe ,nilimsihi aone huruma jinsi ninavyoangaika kuamka alfajiri kupika chapati na mandazi ili tuishi.Nikamwambia nimeona tangazo katika gazeti kuna chuo cha lugha ya kifaransa ambacho ukifanya vizuri unapewa na kazi katika kampuni ya utalii kwanini asisomee! Akacheka sana na kusema hawezi kurudi shuleni kwakuwa ameshakuwa mtu mzima
 
``.Nikamwambia mume wangu asikate tamaa na elimu haina mwisho,nilimbembeleza sana nikamwambia nitamlipia mimi na tena itakuwa hafadhali kwakuwa yeye ni dereva na akisoma na lugha hiyo atapata kazi katika kampuni ya utalii kiurahisi..alinyamaza na baada ya muda nikiendelea kuongea akaanza kukoroma amelala. Niliwaza sana na sikutaka kumuacha mume wangu kwakuwa nilimpenda sana mume wangu.Siku hiyo sikupata usingizi.Palikucha nikadamka kama kawaida nikawasha jiko na kuanza kupika chapatti.Mume wangu aliamka saa mbili na alipotoka kuoga alikuta nimemtengea  chai. Alipokuwa anakunywa chai nikaanza kumweleza tena juu ya kusomea lugha hiyo akaonekana kukubaliana nami  lakini kwa shingo upande.
 
Nilishukuru.Saa sita mchana nilipomaliza kuuza chapati nilikimbia mjini haraka,nikanunua unga wa ngano kilo 20 na vifaa vingine kwaajili ya kupika chapati na maandazi kwa mwezi mzima.Nikiwa nimefungasha vitu vyangu nipo njiani natembea kwa miguu..ghafla nilisikia honi ya gari ikipiga kwa sauti kuu.Nilishtuka na kukimbia pembeni mpaka nikaangusha mzigo wangu niliyouweka kichwani.
 
Wapita njia wakaanza kunisaidia na kunambia..pole..pole nikaitika asanteni jamani. Yule dereva nae alishuka haraka  na kunipa pole.Nikamwangalia usoni kumbe ni Yule baba aliyetaka nimwache mume wangu ili niwe naye ingawa ana mke na watoto.Alinisaidia kubeba mzigo wangu na kuingiza ndani ya gari lake.Nikamwambia asiweke ndani ya gari lake kwakuwa sitopanda gari lake nitakwenda kwa miguu.
 
Alizidi kunisihi nipande gari lake lakini nilikataa..akaingia ndani ya gari na mimi nikabaki nje.wakati huo akiwa ameingia ndani ya gari lake na mzigo wangu.Nilianza kutoa machozi nikitaka anipe mzigo wangu lakini aliendelea kukataa.Tukiwa tunabishana.. `cha ajabu`katikati ya mji mume wangu akatokea akiwa na mwenzake ambaye sikumfahamu.Nilipomwangali nayeye akanaiangalia,kisha akakunja uso..akazidi kunifuata nikiwa nje ya gari lile..Nikamwambia Yule hamza anipe mzigo wangu kwakuwa nipo na mume wangu na huyo hapo anakuja..aliposikia hivyo alitoa mzigo wangu kwa dirishani na kunipa kisha akawasha gari na kuondoka.Mume wangu alipofika akaanza kuniuliza kwa ukali,,Yule ni nani? Nikiwa naanza kujieleza huku natetemeka akanipiga `kofi` nikaanguka chini,,akaanza kunishambulia kwa mateke huku Yule rafiki yake waliyekuwa naye akimzuia asiendelee kunipiga ..Nililia sana na vitu vyangu vilimwagika,unga ukawa haufai tena,mafuta yakamwagika.watu wakaanza kujaa katika eneo la tukio..alinichania sketi na blauzi..kuna akina dada walikuwa na khanga wakaniazima ili nijistiri.mzozo ukaanza huku Yule rafiki yake akimsihii asinipige na badala yake turudi nyumbani kusuluhisha.Watu walijaa na wengine niliwasikia wakisema..``kamfumania mke wake ```.Niliumia sana moyoni kwakweli.Ila kuna baadhi ya watu walioona mwanzo mpaka mwisho wa mimi na Yule mwenye gari walikuwa wakijitahidi kumwelewesha mume wangu kuwa nilikuwa nakataa lifti ya Yule mtu..Nililia sana.
 
Tulirudi nyumbani wote watatu tukiwa na Yule rafiki yake .Nilikaa kitandani huku nalia na kushika kifua changu ambacho nilihisi kimeumia sana.Nikaanza kumwambia mume wangu kuwa Yule mtu alitaka kunipa lifti lakini nilikataa.Mume wangu alifika sana kisha akaniuliza..kama alitaka kukupa lifti mbona aliponiona alitoa mizigo yako ndani ya gari na kukimbia na gari? Nikazidi kumwelewesha kuwa huyo mtu alinipigia honi nikaanguka na ndipo alipotaka kunipa lifti.Mume wangu hakutaka kunielewa,,akazidi kumwambia Yule rafiki yake kuwa mimi namsaliti kwakuwa sasa hana kazi na ndiyo tabia ya wanawake..nilibisha na kujitahidi kumwomba radhi mume wangu.Yule rafiki yake akasema suala lenyewe limejaa utata hivyo anisamehe tu kwakuwa hajanifumania ila alinikuta njiani tena mjini nikiwa na mtu ..Nililia sana nikapiga magoti kumwomba mume wangu anisamehe..alinisamehe lakini akanambia atanifuatilia.nami nikasema nashkuru akinichunguza kwakuwa najiamini kuwa nampenda na sina sababu ya kumsaliti.
 
Tulimaliza mzozo huku mume wangu akiwa amefura kwa hasira.Walitoka na rafiki yake na kuniacha ndani.Mwanangu fatu aliingia ndani na kunikuta nalia .Fatu alianza kulia huku akinikumbatia mimi,Tuliendelea kulia wote,Nilijikaza kiutu uzima na kunyamaza na kumsihi mwanangu fatu anyamaze.Fatu akaniuliza mama unalia nini huku nayeye akiendelea kulia.nilimwambia naumwa na kumwambia anyamaze na aende sebleni.alitii amri yangu.Niliwaza...
 
```nyimbo ambayo sitoisahahu kwa siku hiyo ilikuwa ikipigwa redioni..kiitikio kilisema hivii```matatizoo..yataka kunizidiaa..ooohh..ramaaa...sitovumiliaaaaah..niliimba ile nyimbo mpaka mwisho kisha nikainuka na kwenda kuoga.
JIONI YA SIKU HIYO
Nikiwa na maumivu,nilijitahidi kupika chakula na kuweka mezani,kabla sijala nikameza dawa za maumivu.Ilikuwa ni saa tatu kasoro usiku,mume wangu hakurejea,tulikula na watoto huku yeye chakula chake nikikiweka kabatini.Fatu alianza kusinzia nikamlaza,na abdi alishalala muda mrefu.Ilitimu saa tano usiku mume wangu akiwa bado hajarudi.Nimpigia simu alipopokea niliskia kelele nyingi sana kama vile yupo baa! Nikamuuliza vipi uko wapi mume wangu? Akanijibu kwa sauti ya ukali kuwa nisimsumbue na nimwache ..akakata simu.Nilikosa usingizi mpaka saa kumi usiku bado hajaja.nikapitiwa na usingizi.
 
Nilipoamka siku hiyo sikuweza kupika chapati,sikuwa na unga na pia nilikuwa naumwa kichwa na viungo karibu vyote.Niliamka saa nne kutokana na kuumwa.Nilipoamka nilipika chai nikamtafuta mwanangu Fatu kwakuwa aliamka mapema kwenda katika majumba ya watu ,nadhani alienda kuomba chai huyu mtoto.Nikamwita akaja tukanywa chai.Wakati huo Abdi hayupo kwakuwa alikuwa ni mtundu na nilijua amekwenda kuzurura hasa stendi .Tukiwa tunakunywa chai nilichukua radio yangu na kuweka kanda ya nyinmbo ya zamani.Nyimbo iliitwa `mume wangu`..nikaanza kuimba ili nipate faraja...```mume wangu jerry nimechoka na visa vyako,,,sitovumilia tena kutokana na vituko vyakoo,,nashindwaaa..juzijuzi ulinipiga kukuombaa,,utulie nyumbani.)
 
Tulimaliza chai nikachukua simu kisha kumpigia mume wangu..iliita sana kama dakika tatu hivi haipokelewi..punde ikapokelewa lakini alipokea mwanamke.Nikamwambia naomba kuongea na mwenye simu..akanisunya kisha akaniuliza kwa dharau..kwani we nani? Nikamjibu kwakumwambia mimi mama fatu naitaji kuongea na mmiliki wa hiyo siku ambaye ni Baba Fatu.Akanambia amelala nipige baadaye.Kisha akakata simu.
 
BAADA HAPO!
 
Niliwaza sana na nikaumia sana moyoni,nilikuwa nashika tama muda wote nikiwa chumbani kwangu.Nilikwenda chumbani kwa watoto wangu nikakaa huko kwa muda mrefu.Nilimpigia mume wangu simu kwa mara nyingine saa sita mchana,haikupokelewa hivyohivyo.mchana huo nikapika ugali nikamtafuta fatu tukala. Abdi alishanishinda kutokana na utundu usiyomithilika Nilifanya hivyo kwakuwa Abdi huwa hapatikani mchana ni mtundu ajabu   Baada ya kula nilienda dukani kwa mangi jirani yetu nikamkopa unga wa ngano kila kumi na mafuta ili nianze kupika chapatti asubuhi kisha nimlipe fedha zake taratibu kwakuwa mtaji ulitetereka.
 
Kwa siku mbili Baba Fatu hakutokea nyumbani,ndugu zangu kama kuna kitu kinajua kuumiza hapa ulimwenguni basi ni mapenzi,niliumia sana kwani kila nikipiga simu haipokelewi na kama ikipokelewa basi anapokea mwanamke.Nikiskia sauti ya mwanamke naumi sana najuta kupiga simu na kukaa bila kumpigia mume wangu siwezi.Nabaki kuumia huku nikijiliwaza na nyimbo za akina Marijani Raju,Hemed Maneti na wengineo wa zamani.
 
Siku ya nne Mume wangu alikuja na tulipokaa mezani nikaanza kumuuliza vipi mbona hajaonekana siku nne kuna usalama? Akanambia nisimuulize kwakuwa mimi siyo mwaminifu na ameamua kuoa mke wa pili,tukiwa tunazozana aliingia chumbani na kuchukua begi kubwa na kuweka nguo zake kisha kuondoka kwa hasira.
 
Aliniacha nalia machozi.Usiku uliingia,Abdi alikuja na Fatu tukawa tunakunywa chai  na chapati zilizobaki katika harakati za kuuza.Fautu akaniuliza ``Mama mbona Baba hauypo sikuhizi kwani amesafiri? Nikamjibu ``ndiyo ameenda tena Arusha.Abdi alikuwa akibugia tu chapati bila kuongea `yaonekana alikuwa na njaa na hajulikani alitokea wapi.
 
Pembeni niliweka rekodi ya Bi .Mwanahela ,mwambijai mkongwe wa taarabu mwenye sauti isiyomithilika..nyimbo iliitwa `RABI SINIPE MAPENZI..NA WAPENDWAO HAKUNA,,MAPENZI YA SIKUHIZI WATU KUHADAIANA) nilikuwa naumia sana naposikia nyimbo kama hizo ila ilinilazimu kuzisikiliza kwakuwa nilizipenda na zilinipa ujasiri na nguvu kutokana na mapenzi makubwa niliyokuwanayo juu ya nyimbo hizo.
 
JAMANI MAPENZI  YANAMUUMIZA MAMA FATU……….ANAHITAJI KUNASULIWA..KESHAZAMA..
imeandikwa na mwandishi ma shuhuri wa vitabu mbalimbali hapa nchini  Hemed Kivuyo pia mwandishi huyu ameshaandika kitabu kama rais anamtaka mke wangu pamoja na vingine vingi ukivitaka unaweza kuwasiliana 

Post a Comment

0 Comments