Ticker

6/recent/ticker-posts

WEMA NA DIAMOND PLATNUMZ WAPIGANA LIVE KISA KIMWANA MMOJA WA JIJI FUATILIA HAPA

Stori: WAANDISHI WETU
Tayari kimenuka! Habari ya mjini wikiendi iliyopita ni madai ya njiwa wapendanao Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuchapana makofi laivu, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.

Diamond.
TIMBWILI STUDIO
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyekuwa eneo la tukio, timbwili hilo la haja lilijiri usiku mnene kwenye studio ya kurekodia nyimbo za Bongo Fleva za Tanzania House of Talent (THT) ambapo Diamond alikuwa akirekodi wimbo wa kolabo na msanii wa Kenya, Victoria Kimani ‘Vicky’ na Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz.
Stori ni kwamba wakati wasanii hao watatu wakifanya yao studio, Ommy alichukua kipande cha video kilichowaonesha wakiwa pamoja huku Diamond akiwa ‘veri klozi’ na Vicky kisha akakitumbukiza kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
Wema.
MUVI YAANZA
Hapo ndipo muvi lilipoanzia kwani ilisemekana kuwa Wema ‘Mama la Mama’ alikiona kipande hicho cha video ndipo akaunganisha na ule uvumi wa Diamond ‘kuminya kimalavu’ na Vicky walipokuwa nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Ilidaiwa kuwa Wema alimtafuta shostito wake kwa sasa, Aunt Ezekiel ambaye alimuomba ‘amdraivu’ hadi katika studio hizo lakini yeye (Aunt) hakushuka kwenye gari aina ya Toyota Lexus Harrier la rangi ya pinki.
Mastaa hao wawili ambao wameurudisha uhusiano wao hivi karibuni baada ya awali kuvunjika, walijikuta kwenye ugomvi mkubwa mara tu Wema alipozama studio na kukutana na wasanii hao.
Diamond na Victoria.
UHUSIANO GANI?
Ilidaiwa kuwa Wema alipofika alimhoji Diamond ana uhusiano gani na Vicky huku akimkumbusha kuwa siku chache zilizopita kulikuwa na tuhuma za wao kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Ilisemekana kuwa mzozo huo ulianza taratibu lakini baadaye ulikuwa mkubwa hadi kufikia hatua ya kuchapana makofi huku Ommy na prodyuza Tuddy Thomas wakifanya kazi kubwa ya kuwaamulia bila mafanikio.
UGOMVI SAA MBILI
Kwa mujibu wa ‘kronometa’ yetu, ugomvi huo ulidumu kwa zaidi ya saa mbili huku Diamond akidaiwa kuichukua simu ya Wema na kuipasua chini.
Ilidaiwa kwamba wakati wawili hao wakipeana ‘nakozi’, kila mmoja alikuwa akimtupia mwenzake lugha ‘mbofumbofu’ kama ‘wewe umetembea na fulani’ huku mwingine akimwambia ‘na wewe mbona umetembea na fulani na fulani na fulani na fulani na fulani na…’.
Ilielezwa kwamba kauli hizo zilimfanya Diamond aishie kumwambia Wema kuwa yeye ndiye anamuweka mjini kwa sasa hivyo afunge mdomo wake.
Ilidaiwa kuwa Wema alipoendelea na maneno ndipo Diamond akapandwa na hasira hadi akamchania mwanadada huyo dela sehemu ya mgongoni.
“Asikwambie mtu, palichimbika kweli,” kilisema chanzo hicho.
WAACHANISHWA
Baada ya Ommy na Tuddy kufanikiwa kuwaachanisha, Wema alitoka kwa hasira kisha akatimua. Uzuri ni kwamba hakumgusa Vicky.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimsaka Ommy ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo huku akidai ni masuala ya kawaida katika mapenzi.
Kwa upande wake Diamond simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi (SMS) hakujibu.
WEMA ATOA LA MOYONI
Alipotafutwa Wema, alieleza ya moyoni juu ya sakata hilo ambapo alisema hayo ni mapenzi na ndiyo raha ya mapenzi.
“Kwenye uhusiano kugombana ndiyo raha yenyewe, mapenzi huwa hayaingiliwi nampenda na nitampenda maisha yote.
“Kama ni mjinga, taahira ndiyo tayari amekwishakuwa wangu, kumbuka kuna usemi kuwa chukua jembe ukalime,” alisema staa huyo anayeaminika kuwa maarufu zaidi kwa sasa Bongo.
DIAMOND NA VICKY
Uvumi wa kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na Vicky ulivuma baada ya wawili hao kuonekana kwenye picha ya pamoja wakiwa katika One Project Campaign nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo, wote walikana kwa nyakati tofauti.
SI MARA YA KWANZA
Kuhusu Wema na Diamond kupigana siyo mara ya kwanza kwani jamaa huyo anayeuza zaidi muziki wa Bongo Fleva aliwahi kumtoa nundu mrembo huyo enzi za uhusiano wao wa awali.
Imeandaliwa na Imelda Mtema, Musa Mateja na Shakoor Jongo

Post a Comment

0 Comments