Ticker

6/recent/ticker-posts

UZINDUZI WA MSIMU WA 13 WA MBIO ZA KIMATAIFA ZA KILIMANJARO MARATHON ULIVYOFANA JUZI MJINI MOSHI.





Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akiwa ameshika bendera kuashiria uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni,Uzinduzi uliofanyika Hotel ya Kibo Homes,Wengine ni Viongozi katika kampuni ambazo zimejitkeza kudhamini mbio hizo
Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni,Uzinduzi uliofanyika Hotel ya Kibo Homes,
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli ambao ndio wadhamini wakuu wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2015 ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio hizo uliofanyika Hotel ya Kibo Homes mjini Moshi.
Baadhi ya wageni walikwa katika uzinduzi wa msimu wa 13 wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni uliofanyika mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Kanda ya kaskazini wa kampuni ya Tigo Tanzania ,David Charles ambao ndio wadhamini wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni kilometa 21 akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika mjini Moshi.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mafuta na vilainishi GAPCO ,Caroline Kakwezi ambao ndio wadhamini wa mbio za watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo.
Mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Methacha akizungumza wakati wa hafla ya fupi ya uzinduzi wa msimu wa 13 wa mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kibo Palace Hotels na Kibo Homes ,Vicent Lasway akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika katika Hotel ya Kibo Homes.
Wanariadha toka klabu ya riadha ya Holili wakifuatilia uzinduzi hhuo.

Baadhi ya viongozi walioalikwa katika uzinduzi wa mbio hizo.
Mkurugenzi wa kampuni ya ExecutiveSolution ,Aggrey Mareale akitoa maelezo mafupi kuhusiana na mbio za Kilimanjaro Marathoni ambazo zimeingia msimu wa 13 ,zitakazofanyika mwezi wa tatu mwaka huu.
   

Post a Comment

0 Comments