Ticker

6/recent/ticker-posts

POLISI WADAIWA KUMVUNJA MWANANCHI MIKONO

mkazi wa Loksale Samweli Shani 47,akiwa amefungwa POP baada ya kuvunjwa
mikono yake na polisi,kushoto ni ndugu yake Gabriel Shani akionyesha picha

za Xray alizopigwa zikionyesha jinsi mikono ilivyovunika 
MKAZI wa Loksale wilaya ya Monduli,Samwel Petro Shani(47)amelalamikia
hatua ya kuvunjwa mikono yake miwili kwa kipigo cha askari polisi
katika kituo cha Leskale kwa madai ya kushindwa kulipa deni ya
shilingi 250,000 alizokuwa akidaiwa ana mfanyabiashara wa eneo hilo.
Aidha anawatuhumi askari hao kukodiwa na mfanyabiashara mmoja mkazi wa
eneo hilo kwa lengo la kumshikisha adabu baada ya mkazi huyo kushindwa
kulipa deni la sh,250,000 alizokuwa akidaiwa na mfanyabiashara huyo.
Samweli ameeleza kupokea kipigo hicho ambapo alidai kuwa dhamira ya
askari hao ilikuwa ni kumtoa uhai wake kwani walikuwa wakitumia chuma
kinene kumpiga na kumvunja mikono yake miwili huku mwingine alikuwa
akimshambulia kwa runngu na mateke.
Akizungumza kwa majonzi na gazeti hili jijini hapa,alieleza kuteswa na
askari hao wanaodaiwa kukodiwa na mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina
moja la bi Shamimu,ambaye alikuwa akimdai kiasi hicho cha fedha.
Alieleza kuwa tukio hilo lilitokea februali 6,mwaka huu majira ya saa
3 usiku na kwamba aliwatambua askari wawili waliomtesa kwa kipigo kuwa
ni Steven na Justini wote ni askari wa kituo hicho cha Loksale.
''Mnamo tarehe 6 mwezi huu majira ya saa 3 usiku,walikuja askari
wawili wakiwa wamevaa nguo za kiraia ,walinikuta nimekaa kwenye ukuta
nikiwa na kijana mmoja,walinikamata na kunifunga pingu wakiwa
wamenikandamizia chini ,walinipiga sana na kunivunja mikono yangu
miwili''alisema Samweli
Akisimulia chanzo cha tukio  hilo alisema ,mfanyabishara bi Shamimu
alienda katika kituo hicho cha polisi na kuwaeleza askari hao kuwa
alikuwa akinidai shilingi 250,000 na kwamba sikuwa nimemlipa deni
hilo.
''Ni kweli Shamimu alikuwa akinidai shilingi 250,000 ila nilisha mlipa
shilingi laki moja na kubaki sh,150,000 ,hizo hela kuna msichana
nilimdhamini alikuwa mfanyakazi wa duka lake aliyedai alimwibia ,ndipo
mimi kwa kuwa nilikuwa na mahusiano na msichana huyo nilikubali
kulilipa deni hilo''alisema Samweli
Alisema askari hao walimvamia na kumkaba kabali kisha askari mmoja
alimfunga pingu na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na rungu na chuma
na walipoona wamepoteza fahamu baada ya kumvunja mikono walimkokota
hadi kituo cha polisi na kuendelea kumpigasehemu zingine za mwili
ikiwemo miguuni.
''baadae usiku wakiwa wamenifungia lokapu alikuja mkuu wa kituo na
kuniangalia ,alikuta hali yangu ni mbaya na kuondoka bila kusema
lolote''alisema.
Hata hivyo askari hao waliingiwa na woga kutokana na hali yake na
kuamua kumchukua usiku huo wa manane na kumpeleka katika kituo cha
afya kwa ajili ya matibabu.
Alieleza kuwa kesho yake askari hao walimchukua na kumpeleka kituo cha
polisi wilaya ya Monduli na kumwoka lokapu.Aliongeza kuwa mkuu wa
upelelezi wa wilaya OC CID,aliyemtaja kwa jina moja la bw Abichi
alimfuata akiwa lokapu na kumwambia kuwa anataka ampatie dhamana ila
alitakiwa akibaliane na masharti ya dhamana .
''oc cid aliniambia kuwa nataka nikupatie dhamana ila kwenye maelezo
yako unatakiwa ueleze kuwa ulikuwa unatoroka ulinzi halali wa polisi
ukiwa na pingu ,na wakati ukikimbia ulianguaka na pingu zikakuvunja
mikono yako ''alisema bw Shani.
Aliongeza kuwa hakukubaliana na kauli hiyo ndipo oc cid alipoamua
kumrudisha lokapu ,ambapo alikaa kwa muda wa siku nne wakimbembeleza
akubaliane na maelezo ya polisi .
Alisema kuwa aliamua kuwa na msimamo huo ,hadi tarehe 12 walipoamua
kumfikisha mahakama ya wilaya ambapo alisomewa shtaka ,la kuvunja na
kuiba na kujaribu kutoroka polisi akiwa na pingu ,suala ambalo ni
uongo uliolenga kupoteza haki yake ya kulalamikia jeshi hilo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa alipotafutwa alikiri kupata malalamiko
ya mkazi huyo ,hata hivyo alieleza kuwa kwa sasa yupo likizo ila
aliwasiliana na mkuu wa kituo cha polisi Monduli(OCD)ili kupata undani
wa tukio hilo.
Kwa upande wa mfanyabiashara ,Shamimu alipotafutwa kupitia simu yake
ya mkononi alikana kukodisha askari wa kumpiga na kumvunja mkono
mlalamikaji ila alieleza kuwa yeye alienda kituoni hapo kupeleka
malalamiko yake ,ndipo askari hao walipoamua kumfuata mtuhumiwa na
kwamba kilichotokea huko yeye hafahamu.

 

Post a Comment

0 Comments