Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA NDEGE LA FASTJET LAZINDUA SAFARI MPYA TOKA KILIMANJARO KWENDA MWANZA

 Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akiongea na wandishi wa habari Mkoani Arusha leo wakati wa uzinduzi wa safari mpya ya ndege ya Fastjet kutoka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Kilimanjaro kwenda Entebe Uganda, pembeni  yake kulia ni Lucy Mbogoro Afisa Mahusiano na Masoko  na kushoto ni Neema David Afisa Biashara wote toka shirika hilo.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akimkabidhi tiketi mwandishi wa habari toka Tbc Sechelela Kongola aliyeshinda zawadi ya tiketi ya bure ya kusafiri kwenda Mwanza na kurudi Kilimanjaro wakati wa uzinduzi  wa safari mpya wa shirika hilo toka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Kilimanjaro kwenda Entebe Uganda hafla hizo zilifanyika Mkoani Arusha
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Jimmy Kibati akimkabidhi tiketi mwandishi wa habari toka gazeti la East African Business Week ,Elisha Mayallah  aliyeshinda zawadi ya tiketi ya bure ya kusafiri kwenda Mwanza na kurudi Kilimanjaro wakati wa uzinduzi uliofanyika Mkoani Arusha wa safari mpya wa shirika hilo toka Kilimanjaro kwenda Mwanza na Entebe Uganda.

Post a Comment

0 Comments