Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA KUNUFAIKA NA FURSA ZA AJIRA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA SIMU ZA MKONONI


Vijana wawakikishi wa mitandao 5 katika picha ya pamoja chini ya mnara ...
MAKUNDI ya vijana nchini wanatarajiwa kunufaika na  fursa za ajira kwa
kutumia teknolojia ya simu za mkononi kwa kutumia mfumo mpya wa
kujiunga kwenye mtandao  kwa kuwaingiza vijana wengine ili nao waweze
kunufaika na fursa hiyo.

Aidha mfumo huo utawaunganisha vijana pamoja kwa kuunda mtandao wa
pamoja ambao utawaingiza katika ajira ya moja kwa moja na kuondoa
changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira iliyopo hapa nchini .

Hayo  yalisemwa jana na Mkurugenzi wa kampuni ya Rifaro Afrika mkoani
Arusha, Immaculate Mkodo wakati akizungumza katika uzinduzi wa mfumo
huo kwa mkoa wa Arusha uliofanyika jijini hapa , ambapo alisema kuwa
lengo la kuanzisha mfumo huo ni kuwawezesha vijana kupata ajira na
kuinua uchumi wao.

Mkodo alisema kuwa, mfumo huo wa kutoa ajira kwa kutumia teknolojia ya
simu za mkononi  unatekelezwa na kampuni  ya Rifaro ambayo imeingia
ubia na kampuni ya simu ya Zantel ambayo inawawezesha vijana kupata
ajira  na kipato cha kudumu.

Alisema kuwa, watakaonufaika na mfumo huo ni vijana ambao wamejiunga
na kuwa wanachama  kwa kiasi cha shs  76,500 ,ambapo watapatiwa muda
wa maongezi wa shs 10,000 kwa mwezi ambapo kupitia muda huo wa
maongezi watakuwa wanalipwa kiasi cha fedha kulingana na matumizi
wanayotumia na jinsi watakavyonunua  muda huo .

'kwa kweli mfumo huu ni mzuri sana kwani fedha hizo zitakuwa zinatumwa
kwa njia ya Ezypesa kupitia mtandao wa Zantel huku wakipatiwa kiasi
kingine cha shs 10,000 endapo watafanikiwa kuingiza mwanachama mpya
ambapo kila akileta mwanachama  mmoja anapata shs 10,000 kwa hiyo
akifanikiwa kuingiza  wenzake watano ana elfu 50,000  hela ambayo ni
nyingi sana 'alisema Mkodo.

Mkodo alisema kuwa , mfumo huo utasaidia sana vijana kupata kipato kwa
kutumia vizuri nafasi zao kwani baada ya kuwa mwanachama tu anaanza
kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika kampuni hiyo na hatimaye
 kuweza kuanzisha miradi mbalimbali  ya ujasirimali .

Mwenyekiti  wa  bodi ya ushauri ya Rifaro Afrika, Amenye Mwakisambwe
alisema kuwa , mbali na kuutambulisha mfumo huo mpya wa kupata ajira
kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi pia wameweza kuleta bidhaa
mpya ya kutumia kwenye majiko ya gesi ambayo yanaokoa gharama ya
kubadilisha gesi mara kwa mara na ambapo kifaa hicho hutumika kwa muda
wa  mwaka mmoja .

Alisema kuwa, bidhaa hiyo maarufu kwa jina la 'Gas Saver'  hufungwa
pembeni ya gesi , na kinasaidia sana kuokoa gharama badala ya
kubadilisha mtungi wa  gesi mara 12 kwa mwaka sasa unabadili mara 6
tu kwa mwaka ambapo kwa mwanachama kinapatikana kwa gharama ya shs
72,000 huku kwa asiye mwanachama akipata kwa gahrama ya shs 100,000.

Naye mmoja wa mwanachama aliyenufaika  mfumo huo wa kutumia teknolojia
ya simu za mkononi , Flora Chausa alisema kua , kupitia mfumo huo
ameweza kuwaingiza vijana wenzake na kujiunga katika kampuni hiyo
ambapo ameweza kuanzisha miradi mbalimbali ya ujasirimali na kuondoka
na changamoto kubwa ya ajira iliyopo hivi sasa.

Aidha litoa witio kwa vijana wengine kujiunga kwa wingi katika kampuni
hiyo ili kunufaika na fursa mbalimbali za ajira zilizopo na kujipatia
kipato kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kuweza kujipatia fedha
nyingi kupitia muda wa maongezi utakaotumia.

Post a Comment

0 Comments