Ticker

6/recent/ticker-posts

CWT KUFANYA UCHAGUZI MKUU KITAIFA MAY 28

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  Ezekiah Oluoch akizungumza juu ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kitaifa utakaofanyika Mei 28 katika mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 25 mpaka 28 katika ukumbi wa mikutano wa Ngurudoto,katika mkutano wake na waandishi wa habari jana uliofanyika katika ofisi za mkoa za chama hicho,kushoto ni Katibu wa chama mkoa Hassan Said


Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa May 28 mwaka huu ili kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi  cha miaka 5 pamoja na kutetea maslahi ya walimu.



Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Ezekiah Oluoch amesema kuwa nafasi zinazogombaniwa ni Mwenyekiti wa chama,Katibu,Naibu Katibu mkuu pamoja na Mhazini wa chama hicho.



Ezekiah alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za  chama hicho Mkoa wa Arusha kuwa hadi sasa wana jumla ya wanachama  452 wamejitokeza kugombea nafasi hizo  na nafasi nyingine ikiwamo Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu  ,na kitengo cha Walimu wanawake.



“Wagombea ni wengi na nafasi ni chache tumeona tuache hivyo maana yake tukizuia idadi tutakua tumeminya demokrasia” Alisema Ezekiah



Ezekiah amesema kuwa jumla ya walimu 1000 wanatarajia  kushiriki uchaguzi huo wa kitaifa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.



Mwenyekiti wa Chama hicho  Mkoa wa Arusha (CWT) Jevin  Buruya amesema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi huo hivyo amewataka walimu wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi huo.



Jevin amesema kuwa Chama cha Walimu Tanzania kitafanya mkutano mkuu utakaoanza May 25 hadi 28 ambapo agenda kuu ni Uchaguzi Mkuu,Mkutano huo unatajwa kuwa Mkutano wa Mwisho wa Raisi Kikwete kuwahutubuia walimu

Post a Comment

0 Comments