Ticker

6/recent/ticker-posts

GOLA YAANZISHA JUKWAA LA KIONGOZI TUNAYEMTAKA

Taasisi isiyo ya kiserikali  ya Gola iliyoko jijini Arusha imeanzisha Jukwaa la Kiongozi tunayemtaka linalotoa elimu ya uraia kwa  itakayowasaidia wananchi kupata viongozi bora watakaosukuma gurudumu la maendeleo ya nchi.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Elisha Maghembe amesema kuwa tayari wameanza kuyakutanisha makundi mbalimbali ikiwemo Wananchi na  Vyama vya siasa na kufanya midahalo mbali mbali ambayo inawajengea uwezo wananchi kujua kiongozi gani anayefaa kuwaongoza.

“Tunapoelekea uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu elimu ya uraia ni muhimu tunawaambia wananchi wasikubali kulubuniwa na kuchagua viongozi wabovu watakaoligharimu taifa letu” Alisema Maghembe

Elisha alisema kuwa wamefanya midahalo katika baadhi ya kata zilizoko jiji la Arusha ikiwemo Kaloleni,Sekei,Kijenge,Ungalimited huko wamehamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi kwa kujiandikisha na kupiga kura kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Alisema kuwa miongoni mwa vyama vya siasa ambavyo wamekutana navyo na kufanya midahalo na majadiliano ni pamoja na CHADEMA ,CCM na CUF bado wanaendelea na juhudi za kukutana na vyama vingine.

“Kumekua na sintofahamu ,Vyama vinawaweka wagombea ambao wananchi hawawataki ,midahalo hii inasaidia vyama vya siasa kukutana na haja za wananchi na pia kufanya kampeni kwa amani na utulivu pindi wanapoanza mchakato wa uchaguzi” Alisema Elisha

Jukwaa hilo linatarajia kuwasaidia wananchi kuwapata viongozi makini ,viongozi bora kuanzia ngazi ya chini ya madiwani,wabunge mpaka Raisi.

Post a Comment

0 Comments