Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUMIZI MABAYA YA ARDHI TISHIO KWA UHIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu 
Na Woinde Shizza,Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi
mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi
yamekua tishio kwa  maeneo uhifadhi hivyo kupelekea uvamizi wa maeneo
hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo kinyume cha
utaratibu.
Nyalandu amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kati ya
Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) uliofanyika jijini
hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu  utakaorithiwa na
vizazi vijavyo  mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi
kuzingatiwa.
Waziri huyo amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi
ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi
hivyo amewataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji  kwa kuwekeza
nje ya hifadhi.
“Mtu anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu
vizuri  lazima tutawanye  uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi”
Alisema Nyalandu
Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za
Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya
nyingine  17 ziko katika hatua mbalimbali za uanzishwaji,amezitaka
jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi katika
kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanayama pori ya mwaka
1998.
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard  Chambulo
alisema kuwa ili uhifadhi uweze kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na
hati miliki za maliasili ili waweze kuzitunza vyema.
Chambulo anaeleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni
nguzo muhimu sana kwa uhifadhi  itakayosaidia kuwa na utalii endelevu
kwa vizazi na vizazi.

Post a Comment

0 Comments