Ticker

6/recent/ticker-posts

MADEREVA BODABODA WATAKIWA KUINGIA DARASANI KUSOMA ILI KUPUNGUZA AJALI ZA MARA KWA MARA

 picha maktaba  ya madereva toyo
Na Woinde Shizza,Arusha

Waendesha bodaboda wametakiwa kukwenda kwenda darasana kupata elimu ya usalama barabarani ili kuweza kuepusha ajira za maramara kwa mara zisizo tarajiwa .

Haya yalibainishwa na diwani wa viti maalumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Usariver Mary Antony  wakati akiongea na madeva bodaboda hao mara baada ya kuwalipia  ada ya mafunzo ya usalama barabarani madereva 45 wa kata ya usa river.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila dereva bodaboda kwenda kupata elimu ya usalama barabarani ili kuweza kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara kwa kusababishwa na uzembe wa madereva hao.
“mimi kama diwani wa viti maalumu niliamua kwenda kuwapatia kuwalipia ada ya mafunzo  madereva hawa wa bodaboda ili angalau waweze kujua sheria za barabarani na pia waweze kupata leseni maana hawa wote awana lesini na sio ivyo tu nadhani iwapo madereva hawa watazijua izi sheria za bara barani hii itasaidia kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zinatokea”alisema Mary

Alibainisha kuwa ni wajibu wa kila dereva kujua sheria na iwapo atajua sheria  watajiamini na pia awatasumbuliwa ata na polisi  wa usalama barabarani njiani kwani watakuwa wanajua sheria hivyo ata akiambiwa amefanya kosa ataweza kujua ni kosa kweli au amedanganywa kwakuwa tayari anajua sheria hizi za usalama wa barabarani.

Kwa upande wake mmoja wa vijana wa bodaboda wa kata hiyo ya Usariver alisema kuwa anamshukuru diwani huyo kwa kuwasaidia kwani wamejitambua  na wajua sheria na aliwasihi madereva wenzake kwenda mashuleni kujua sheria hizo.

Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo wameyapata yatawasaida kujiamini  na pia yamewasaidia pia kutowaogopa  askari wa barabarani kama zamani kwani kwa sasa wanajua sheria ya usalama barabarani na sio hivyo tu katika mafunzo hayo pia wamefundishwa mafunzo ya ulinzi shirikishi ili kuwezakuwatambua wezi  na jinsi ya kujiepusha na wateja ambao hawawaeliwi kwani kipindi hichi madereva wengi wanaibiwa pikipiki zao.

Post a Comment

0 Comments