Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATAKIWA KUFUNGUA OFISI ZA UTALII KATIKA NCHI AMBAZO ZINALETA WATALII WENGI HAPANCHINI NA KUPUNGUZA VIINGILIO VYA WAGENI ILI KUSAIDIA KUPATA WAGENI WENGI AMBAPO WATASAIDIA KUKUZA PATO LA TAIFA


 Afisa usiano wa chama cha waajiri  (ATE) Patricia Chao akiwa anawapa maelekezo baadhi ya wateja wakigeni waliouthuria katika banda lao kujua jinsi  ili kuweza kujua jinsi chama cha waajiri kinavyofanya kazi








Afisa usiano wa chama cha waajiri  (ATE) Patricia Chao akiwa anawapa maelekezo baadhi ya wateja wakigeni waliouthuria katika banda lao kujua jinsi  ili kuweza kujua jinsi chama cha waajiri kinavyofanya kazi

  Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi  Gibson Olemeiseyeki akipata maelekezo ya  huduma zinazotolewa na kampuni ya utalii  OSUPUKO nature Paradise iliopo mkoani Arusha


 Emma Saria   Treasury  Dealer wa benki ya ABC akiwa anawaonyesha wateja waliouthuria katika banda lao aina tofauti tofauti za kadi za benki zinazotolewa na banki yao

 Meneja wa Banki ya ABC Joyce Malai akiwa anawapa maelezo ya huduma zinazopatikana katika benki yao na jinsi ya kufungua akaunti ndani ya benki yao ambapo alisema kuwa kima cha chini cha kufungulia akaunti ndani ya benki yao ni shilingi 5000 na benki yao inatoa huduma ndani ya nchi na nje kwani ni ya VISA na pia unaweza kulipia kitu chochote ukiwa na kadi yao ATM card


 meneja wa Banki ya Banc ABC  yenye tawi lake  Arusha karibu na hospitali ya ST.Thomasi Mbuche Zambi akiwa anaongea na wateja (hawapo katika picha) waliouthuria banda hilo

 wananchi wakiendelea kupata maelezo ya utalii ndani ya banda la Ngorongoro Conservation lililopondani ya maonyesho hayo




 kikundi cha ngoma kikiendelea kutumbuiza


 wamama wa kimasai wakiwa wamekaa wanaangalia burudani mbalimbali za vikundi vya ngoma
kikundi cha ngoma kutoka morogoro kikiendelea kutumbuiza ndani ya baadhi ya mabanda yalikuwepo katika maonyesho


Habari picha na  Woinde Shizza,Arusha



Serikali  imetakiwa kufungua ofisi za utalii katika kila nchi  ambazo zinaleta watalii hapa nchini pamoja na kupunguza viingilio vya wageni wanaotembelea hifadhi zetu za taifa ili kuweza kuongeza idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini  .



Hayo yamebainishwa na mbunge  Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi  Gibson Olemeiseyeki wakati alikuwa akiongea na waandishi wa habari alipotembelea katika maonyesho ya utalii ya Karibu fair yanayofanyika ndani ya viwanja ya magereza nje vilivyopo ndani ya jiji la Arusha .



Alisema kuwa  serekali inapaswa kufungua ofisi katika kila  nchi ambayo inajua inaletawageni hapa nchini ili kuweza kutangaza utalii wetu vizuri,na ili kuweza kupata wageni wengi zaidi  ambapo wakiingia kwa wingi watasaidia kuongeza pato la taifa na kupunguza tatizo la ajira kwani vijana wengi wanaweza kujiajiri kupitia utalii pamoja na biashara za utalii .



Alibainisha  kuwa ni jambo la ajabu nchi kama Tanzania ambayo inavivutio vingi vya utalii  huku ikiwa  ni nchi mojawapo ambayo iko katika nchi kumi bora ambazo zinaongoza kwa kuwa na vivutio vya utalii lakini ni nchi ambayo inaongiza watalii wachache sana ukilinganisha na vivutio vilivyopo.



“nchi kama Tanzania pamoja  na vivutio vyote lakini kwa mwaka tunaingiza watalii milioni moja  wakati nchi kama maleshia kwa mwaka wanaingiza watalii miolini 15 ni jambo la kushangaza alafu ukiwaangalia viongozi wetu badala ya kukaa na kuangalia jinsi ya kufanya ili wataliii wangie na wawe wengi lakini wao wanakaa wanachekelea na wanafanyakazi ya kuongeza ada ya kuingia katika ifadhi yetu kila mara sasa hiii kweli si itakimbiza wageni badala ya kufanya wageni waongezeke kila siku”alisema Olemeiseyeki



Alisema kuwa kupitia utalii serekali inaweza kuingiza ela nyingi sana na sio ola pia inaweza kuwaachiri vijana wengi sana  ,iwapo ikijipanga  vizuri  na kutumia fursa vizuri kwani kama nchi zingine zinaweza ata serekali yetu itaweza iwapo tu itaajiri wafanyakazi ambao wanauchungu na hifadhi zetu na pia wanataaluma ya kutosha kuhusiana na utalii na sio kuajiri watu ambao awana taaluma na kuajiri watu kiundugu undugu na kiubinamu.



“unajua ukiona bidhaa aina soko unatakiwa uishushe bei na uangalie nini cha kuboresha ili uweze kuuza bidhaa yako sasa apa kwetu viongozi wanapandisha bei kila siku awaangalii ni chakufanya ili utalii na watalii waje kwa kasi hapa nchini badala yake wanapandishi kila kitu sasa kibaya zaidi ata bei za ndege ambazo zinaleta wazungu zikitaka kutua hapa kuleta watalii yaani wanapangiwa garama kubwa mno kiasi kwamba wanashindwa kuja inabidi waende katika nchi jirani ya Kenya wakatue maana wenzetu wanatambua umuimu wa kushusha bei na ukiangalia sasa ivi pamoja sisi tuna vivutio vingilakini nchi ya Kenya inajulikana kuliko nchi yetu Tanzania ambayo inavivutio “alisema Olemeiseyeki


Aidha alimalizia kwa kuitaka serekali kupunguza tozo za utaliii pamoja na kuraisisha ujaji wa wageni hapa nchini ili kuweza kukuza ongezeko la watalii hapa pamoja na kuboresha miundo mbinu ndani ya hifadhi zetu.



Kwa upande afisa usiano wa chama cha waajiri  (ATE) Patricia Chao alisema kuwa maonyesho ni mazuri  na  kwani muamuko upo kwani watu wameuthuria tofauti na kipindi kingine  kwani amewaona washiriki wengi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo kenya ,uganda ,Rwanda ,Burundi na hata South Afrika tofauti na kipindi kingine.



“kiukweli maonyesho ni mazuri lakini pia naisi ukosefu wa fedha ndio umefanya pia wamiliki wengi wa utalii kutokuja kuonyesha bidhaa zao kwa sababu nyie wenyewe waaandishi mmeona hamda kampuni kama Leopard tours ,sopa lorge pamoja na serena hii inaonyesha ni jinsi gani sasa ivi hela hamna na ukiangalia garama pia ya kuwa na banda hapa ni kubwa sana sasa mtu akiangalia anaona kuliko apoteze fedha yake bure ni bora asije kuonyesha kwakweli napenda kutumia mda huu kuwasihi waandaaji wa maonyesho haya kupunguza garama za kuwanabanda hapa pamoja na hata ya kiingilio siku ya kwanza ili kila mmoja awe ze kuja na kujionea “alisema Afisa biashara wa Serena hotel Jonathan Njotto.



Post a Comment

0 Comments