Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOIZI WA KIMILA JAMII YA KIMASAI ARUSHA WABANWA


Na Woinde Shizza, Arusha 

Viongozi wa kimila  jamii ya kimasai  maarufu kwa jina la Laigwanani wametakiwa kuacha kujiingiza katika maswala ya kisiasa kwa kutumiwa na wanasiasa ili kudumisha mila na desturi za kabila ilo .

Aidha viongozi hao wameaswa kuhamasisha jamii ya kabila hilo kuwapeleka watoto wao shule ili kupata elimu itakayo wasaidia kukabiliana na changamoto za kimaisha ikiwemo swala la ajira ambalo ni tatizo   kubwa kwa jamii hiyo ya kifugaji .

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Arusha na mwenyekiti wa Laigwanani .Isac l LeKisongo katika kikao maluum cha kutambulisha uwongozi mpya uliochaguliwa hivi karibuni wilayani Monduli kilicho jumuhisha Laigwanani kutoka wilaya 6 za mkoa wa Arusha.

Elkisongo alisema kuwa wanasiasa wamekuwa changamoto kubwa katika jamii ya kimasai kufuatia baadhi ya malegwanani wakijikuta wakishawishika na wanasiasa na kuweka pembeni mila na desturi za kabila hilo zinazo wataka wasijingize kwenye maswala hayo kwakuwa walichaguliwa kwa hajili ya kuwatumikia wananchi wote .

Mwenyekiti huyo ambaye amechaguliwa kuwaongoza vingozi wa kimilaamesema atakikisha anasimamia misingi ya kabila hilo kwa kurejesha eshma ya kabila hilo ambayo imeanza kutishia kupotea na kuihasa jamii ya kabila hilo kudumisha mila yao na kuzingatia kuwapeleka shule watoto wao.

Naye mwenyekiti wa malegwanani tawi la Monduli Mepukori Mberekeri, alilaani hatuwa ya vijana wa kimasai kukimbilia mjini na kujiusisha na maswala ya kusuka nywele ulinzi,na kukata kucha wakina mama na kudai kuwa kitendo hicho kinazalilisha kabila hilo na kueleza kuwa yeye pamoja na viongozi wenzake watangalia uwezekano wa kuchukuwa hatuwa .

Akizungumzia swala la viongozi wa mila kujingiza katika siasa amesema tayari wameshaanza kuchukuwa  hatua ya kuwatoza faini ya dume moja la Ng’ombe wale wote walotekwa kisiasa na kusababisha mgawanyiko kwa jamii hiyo.
Aidha alisema swala la viongozi katika jamii hiyo kwa sasa ni gumu na awafikirii kumpa rungu mwanamke kama eshma ya jamii hiyo kuongoza wanaume isipokuwa wameruhusu wakina  mama wa jamii hiyo kujingiza  katika maswala ya kisiasa kushika nyazifa mbali mbali wazitakazo.

Viongozi hao waliochaguliwa wanatarajiwa kusimikwa na kupewa eshma juni 3 mwaka huu katika sherehee zitakazo fanyika katika ofisi zao zilizopo eneo la chuo cha ufundi Arusha

Post a Comment

0 Comments