Ticker

6/recent/ticker-posts

GOOGLE YAZINDUA PROGRAMU MPYA KWA JINA LA DUO


Programu hiyo ni jibu la Google kwa programu nyengine kama ile ya Apple
ya Face Time,Skype ya Microsoft na Facebook messanger.

Haina tofauti kubwa na programu nyengine zinazotoa huduma za
video,isipokuwa inakupatia uwezo wa ni nani anayepiga simu hivyobasi
kumpatia mtumiaji fursa ya kuamua iwapo ataipokea simu hiyo au la.

Google inasema kuwa programu hiyo imetengezwa hali ya kwamba
inakubishia hodi kabla simu kuingia.

Programu hiyo mpya iliotangazwa mwezi Mei inazinduliwa kama huduma ya
bure kwa simu zinazotumia Android pamoja na simu za Apple za iPhone.

Simu zinalindwa na haziwezi kudukuliwa na video hubadilika kulingana na
kasi ya kushika simu inayopigwa.

Kama programu ya FaceTime ,duo inahitaji nambari ya mtu ya simu
kuunganishwa.

Huduma nyengine zinahitaji mtumiaji kuingia katika akaunti zao ili kupata
fursa ya kupata huduma hiyo.





Post a Comment

0 Comments