Ticker

6/recent/ticker-posts

TRA YAZINFUA KAMPENI YA UHAKIKI WA NAMBA ZA MLIPA KODI (TIN)

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara katika
jiji la Dar es salaam kuboresha taarifa za usajili wa namba ya
utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ili kuondokana na mfumo wa kizamani
wa usajili wa namba hiyo.

Uhakiki huo utaiwezesha mamlaka hiyo kuweza kujua idadi sahihi ya
wafanyabiashara walipa kodi, kuondoa walipa kodi hewa ambao
wamekuwa hawajihusishi na biashara kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo vifo au kufungwa kwa makampuni yao.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidata alisema
mfumo huo utawawezesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa gharama
nafuu sambamba na kuweka mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari.

Kidata alisema kuwa mfumo wa sasa wa uhifadhi kumbukumbu za
walipa kodi ulikuwa na kasoro nyingi hivyo mfumo mpya utaendana na
ukuaji wa teknolojia na kukuza uchumi.

“Zoezi hili linamtaka kila mwenye namba ya utambulisho yani TIN kufika
katika ofisi za TRA zilizopo karibu naye bila kuwakilishwa na mtu yeyote
na zoezi litatumia dakika 10 kumalizika” alisema
Naye Elija Mwandubya ambaye ni kamisha wa mapato wa ndani wa
mamlaka hiyo, alisema zoezi hilo litachukua siku 60 na kuanzia Dar es
salaam na baadaye kuhamia mikoa mingine ndani ya nchi.

“TRA ina wafanyabiashara walipa kodi milioni mbili na laki moja hivyo
uboreshwaji wa TIN utatupa uelewa wa idadi kamili ya walipa kodi”
Alisema
Elija alisema kutakuwa na vituo maalum kwaajili ya uhakiki wa taarifa
katika mikoa ya kikodi ambapo Kinondoni wafanyabiashara watatakiwa
kutembelea ofisi za TRA zilizopo jengo la LAPF – Kijitonyama na Kibo
Complex Tegeta.

Ilala wafanyabiashara watembelee ofisi ya TRA shauri moyo na 14 Rays
Gerezani na Temeke wafike ofisi za uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments