Ticker

6/recent/ticker-posts

MWANDAAJI WA MISS TANZANIA KANDA YA KASKAZINI ABWAGA MANYANGA



katika picha ni aliyekuwa mwaandaji wa shindano la Miss Kanda ya Kaskazini Faustine Mwandago ,mwandaaji huyu anastalii pongezi kwani ni mwaandaaji wa kwanza kuandaa mashindano ya urembo kwa kanda ya kaskazini na kutusaidia kufanikiwa kupata mrembo anaewakilisha Tanzania  ambaye ametokea mkoa wa Arusha

Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog  Arusha
Mwandaji wa tamasha la Miss Tanzania kanda ya kazkazini ambaye pia ni
mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Entertainment Ltd,Faustine Mwandago
ametangaza kujiondoa rasmi kuandaa tamasha hilo huku akitaja sababu
iliyompelekea ni pamoja na ubabaishaji uliojaa ndani ya mashindano
hayo.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa Mwandago alisema
kwamba ameamua kuchana na kuandaa tamasha hilo kutokana na hali ya
ubabaishaji iliyokithiri ndani ya mashindano hayo.
“Nimeamua kuachana na kuandaa tamasha hili kwa kuwa kuna mambo ya
ubabaishaji mwingi ndani yake kadri ya siku zinavyokwenda mambo
yamekuwa na ubabaishaji sana umesikia hata Mwanza yaliyotokea
yanakatisha tamaa”alisema Mwandago
Alisema kwamba   mbali na sababu hiyo jambo jingine lililompelekea
kuachana na uandaaji wa tamasha hilo ni pamoja na uhaba wa wadhamini
ambao umeshuka kwa kikubwa na kupelekea kudhohofisha mashindano hayo.
Mwandago,alisema kwamba lakini pamoja na kuachana na kuandaa tamasha
hilo atakuwa bega kwa began a mshiriki wa taji hilo kanda ya kazkazini
katika safari yake na kumtaka mlimbwende huyo kutokuwa na wasiwasi.
“Pamoja na kwamba nimeamua kuachana na  kuandaa tamasha hili lakini
mrembo anayewakilisha kanda ya kazkazini ambaye nilisimamia uteuzi
wake nitaendelea kumpa sapoti katika safari yake bila wasiwasi”alisema
Mwandago
 

Post a Comment

0 Comments