Ticker

6/recent/ticker-posts

SHAKA HAMDU SHAKA AKUTANA NA MKUU WAMKOA WA SIMUYU NA KUZUNGUMZA JINSI YA KUWEZASHA VIJANA KUMUDU KUWEZA KUJIAJIRI


 Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe:Antony Mtaka akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mapema
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Banda na kupata Naelezo Mbali mbali juu ya Shughuli mbali mbali zinazofanywa Jeshi la Kujenga Taifa Kambi ya Msange
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akipata Maelezo katika Banda la NHIF

 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akimweleza jambo  Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe Antony Mtaka  kwa Msisitizo
 
Viongozi wakishikilia bidhaa zinazozalishwa na Vijana Mkoani Simiyu

Na Woinde Shizza wa Globu  ya jamii

Katimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu  (MNEC)   amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu Mhe, Antony Mtaka ofisini kwake Bariadi Mkoa wa Simiyu katika mazungumzo yao waligusia Nyanja mbali mbali za kuimarisha mfumo wa kuwawezesha vijana kumudu kujiajiri ikiwa ni kupunguza malalamiko ya kilio cha ukosefu wa ajira kwa vijana. Kaimu Katibu Mkuu amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa  kuitikia na kutekeleza kwa vitendo agizo la  Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda ili kutoa fursa kwa vijana kupata ajira.



Amesifu mpango mkakati na utekelezaji wake unaojulikana Wilaya mmoja kiwanda moja ni kampeni ambayo imeanza kuonyesha matukio ambapo vijana wanaonekana kuanza kuchangamkia fursa hiyo ndani ya wilaya za mkoa wa Simiyu, ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa wengine kuiga mfano mzuri ulioaznishwa na Mkoa wa Simiyu ili kuendana kwa pamoja na kasi na lengo la Rais la HAPA KAZI ambapo kinadharia linahimiza maendeleo endelevu nay a haraka katika sekta zote za kiuchumi  na kijamii hususan kwa Vijana.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemueleza Kaimu katibu Mkuu Shaka kuwa wamejipanga vizuri katika kubuni na kuendeleza mipango yao sio kwa maneno bali kwa vitendo ili kuufanya mkoa huo kuwa  kitovu  cha viwanda vidodogo na vya kati na viwanda vikubwa . Kwasasa Simiyu imeanzisha kiwanda cha maziwa Wilaya ya Meatu na kiwanda cha Wilaya ya Maswa



Wakati huo Kaimu Katibu Mkuu ametembelea na kukagua mabanda ya Maonyesho yaliyozinduliwa tarehe 7 mwezi huu ikiwa ni miongoni mwa shuhuli za wiki ya Vijana kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.Kaimu Katibu Mkuu ameridhishwa na muamko wa vijana katika kuonyesha muamko wa kuitikia wito wa Serikali wa kuwekeza katika miradi yao ya kijamii ili kumudu kujiari na kupunguza kilio cha ukosefu wa ajira sambamba na kuwanusuru wasijiingize katika matendo maovu.



Post a Comment

0 Comments