Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKOSA YA UBAKAJI YAPUNGUA MKOANI ARUSHA

Related image

 Na Woinde Shizza,Arusha

MAKOSA ya ubakaji wa watoto na wanawake katika mkoa wa Arusha
yamepungua kutoka makosa 164 kwa kipindi cha January hadi septembar
2015 hadi kufikia makosa 108 kwa kipindi cha January  hadi September
2016 kutokana na  elimu inayotolewa kwa jamii  kuhusiana na namna ya
kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia unaofanywa kwa wanawake na
watoto.

Aidha kwa upande wa kesi za kulawiti kwa mwaka 2015 jumla ya makosa 41
yaliweza kuripotiwa kituoni huku kwa mwaka 2016 makosa 26 ya kulawiti
nayo yakiwa yameripotiwa hivyo takwimu kuonyesha kuwa vitendo hivyo
vimepungua tofauti na mwaka jana.

Hayo yalisemwa na mkuu wa kitengo cha polisi  dawati la jinsia na
watoto Happy Temu alipokuwa akizungumza katika mdahalo
uliowashirikisha wanafunzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wa
siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika chuoni hapo.

Alisema kuwa kama dawati la jinsia wamekuwa na nafasi kubwa ya
kupunguza ukatili wa kijinsia ambapo kutokana na takwimu hizo
wamefanikiwa kupunguza tatizo la ubakaji kutokana na juhudi ambazo
jeshi hilo kupitia dawati la jinsia wamekuwa wakikabiliana nalo katika
kupunguza ukatili wa kijinsia ambao wamekuwa wakitendewa wanawake na
watoto.

“makosa 164 ya ubakaji kwa 2015 yaliweza kuripotiwa lakini kwa mwaka
huu 2016 tunaona takwimu kuwa makosa 108 ndio yaliyoripitiwa hivyo
tunaona wazi kuwa makosa ya ubakaji yamepungua nah ii inatokana na
elimu tunayoitoa kwani tayari tulishaanza kutoa elimu ya ukatili wa
kijinsia  kwenye shule zetu za msingi kwani tuligundua kuwa watoto wa
hizi shule wanafanyiwa sana ukatili wa kijinsia na hivyo makundi haya
tayari yameshaelimika kwani bado tuna mpango wa kuendelea na utoaji wa
elimu katika shule zetu zote “aliongeza Happy.

 Mratibu wa kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya
wanawake cha  Tanzania kilichopo katika tasisi ya maendeleo ya jamii
tengeru  ,   Ebeneza  Lauwo,  alisema kuwa kutokana na vitendo vya
ukatili kuzidi kushamiri wameamua kuandaa mdahalo huo ili kujadili kwa
pamoja na wanafunzi hao  kupinga siku 16 za ukatili wa kijinsia  kwa
kujadili kwa pamoja maswala ya ukatili wa kijinsia na kuweza kubaini
tatizo limekuwa kubwa kiasi gani kwa jamii.

Alisema kuwa lengo la kuadhimisha siku 16 za ukatili  ni kuibua
matatizo ya ukatili wa kijinsia na kuweka mikakati ya kutokomeza na
hivyo kuanzia mwakani watatoa mafunzo  kwa jamii kuanzia ngazi za
chini namna ya kuthibiti vitendo vya ukatili ambao wanaishi na watu
wanaofanyiwa hivyo vitendo ili hadi ifikapo mwaka 2030  waweze kuingia
kwenye maendeleo  endelevu.

“tuna takwimu za kitaifa za ukatili  ambapo kwa mwaka jana tulikuwa na
visa elfu 3108 na mwaka huu kuna visa 1777  ambazo zinapatikana nchi
nzima na hizi tarifa tunaziweka kwenye kituo ili ziweze kutumika na
hivyo bado tatizo ni kubwa kwa nchi nzima hivyo ipo haja ya elimu
zaidi kutolewa ili kuthibiti vitendo hivi”aliongeza Lauwo.

Mhadhiri wa taasisi ya maendeleo ya jamii Jackson Muhoho alisema kuwa
mamlaka ya rais ikitumiwa vizuri itawezesha kukomesha ukatili wa
kijinsia kwa kuwa yeye ni mbunge namba moja ya mwenye mamlaka ya
kutunga sheria na kutoa matamko kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya
muungano ya kuthibiti vitendo vya ukatili kama ilivyo matukio mengine
kwenye jamii.

Baadhi ya wanafunzi hao wakizungumza katika mdahalo huo waliiyomba
serikali kuhakikisha kuwa kwa inatunga sera ambazo zinatekelezeka
kwani zipo sera ambazo hadi sasa hazitekelelzeki hivyo kusababisha
vitendo vya ukatili kuendelea kushamiri.

Post a Comment

0 Comments