Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI HOTELI YA PARROT ARUSHA WALILIA MALIMBIKIZO YA MSHAHARA WAO




Baadhi yawafanyakazi wa hoteli ya kitalii ya Parrot iliyopo
katikati ya jiji la Arushawameulalamikia uongozi wa hoteli hiyo
kuwatelekeza jijini hapa na kushindwa kuwalipamalimbikizo ya mshahara
yao ya zaidi ya kiasi cha sh,50 milioni tangu mwaka jana.
Mbali na malimbikizohayo wafanyakazi hao wamedai fedha za malimbikizo
ya Nssf zaidi ya kiasi chash,15 milioni sanjari na kufukuzwa katika
hoteli ya Royal Court iliyopo Sakinajijini hapa ambapo uongozi wa
hoteli hiyo uliwakodishia kama sehemu ya malazi .
Wakizungumza kwanyakati tofauti wafanyakazi hao walisema ya kwamba
waliletwa jijini hapa mweziOktoba mwaka jana kutoka mikoa mbalimbali
nchini kwa lengo la kuja kufanya kazi lakini kinyume chake uongozi wa
hotelihiyo umeshindwa kuwalipa mishahara yao na sasa umewafukuza kazi
kinyemela.
David Sichinga ambayeni meneja mapokezi alisema kwamba waliwasili
mwezi Otoba mwaka jana nakukodishiwa sehemu ya malazi katika hoteli ya
Royal Court lakini cha ajabuuongozi wa hoteli hiyo umekuwa ukiwapiga
danadana kuwalipa mishahara yao tangumwaka jana.
Ezra Ezekiel ambaye nimeneja utunzaji nyumba alisema kwamba yeye
ametokea mkoani Mwanza na hali yamaisha imekuwa ni ngumu jijini Arusha
kwa kuwa hajui anakula nini wala kulalawapi huku akisisitiza  ameacha
familia mbaliambayo inamtegemea.
“Mimi nilichukuliwakutoka mkoani Mwanza nikaletwa kufanya kazi hapa
Arusha lakini cha ajabutumetelekezwa na sijui nitakula nini wala
kulala wapi kwani tumefukuzwahotelini na kazini tumeambiwa
tusikanyage”alisema Ezekiel
Naye, Benedict Machageambaye ni meneja wa chakula na vinywaji mkazi wa
jijini Dar es salaam    alisema kwamba wanaiomba serikali
kuingiliakati madai yao kwa kuwa wanahisi ya kwamba uongozi wa hoteli
hiyo unalenga kuwaporahaki zao.
Machage, alisema kwambakuna baadhi ya wafanyakazi wametoka kisiwani
Zanzibar na hawajalipwa hata sentitano tangu wawasili jijini Arusha
kufanya kazi huku akidai hali yao kimaishaimekuwa ngumu.
Mkurugenzi wa hotelihiyo ,Abdallah Mshana alipoulizwa na gazeti
hilikuhusiana na madai hayo alisema kwamba anawatambua watu hao kama
waliwahikufanyiwa usaili na sio kuajiriwa huku akiwataka waende
mahakamani endapo wana malalamiko.
“Mimi natambua kwambahao watu waliwahi kufanyiwa usaili na sio kwamba
waliajiriwa na kama wanamalalamiko waende mahakamani”alisema Mshana
Hatahivyo,mkurugenzi mtendajiwa kampuni ya Hospitality Concepts
International ambayo imepewa jukumu lakuajiri wafanyakazi hao na
kusimamia hoteli hiyo  ,Macmillan Simba alikiri kuwatambuawafanyakazi
hao na sanjari na madai yao ya mishahara na Nssf na kusemakwamba kuna
matatizo ya kifedha yanayowakabili na pindi yakitatuliwa watalipwa
tufedha zao.
Simba,alisema kwambawaliwajulisha wafanyakazi hao kurejea makwao
mwishoni mwa mwaka jana kutokanana matatizo hayo ya kifedha lakini
baadhi yao waligoma na kuhusu kutimuliwahotelini alikiri suala hilo na
kudai kwamba wameshatangaza mgogoro na mwajiri wao na hivyo ni vigumu
mwajiri huyo kuendelea kuwalipia hoteli.

Post a Comment

0 Comments