Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA GOODALL FOUNDATION YAPONGEZWA KUWEZA KUINUA ELIMU YA JUU

Image result for MKUU WA WILAYA YA ARUSHA

MKUU wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro amempongeza Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Goodall Foundation ya Uingereza, Andrew Goodall kwa kuamua kutumia fedha zake kuboresha elimu hapa nchini.

Goodall ametumia fedha zake kuinua elimu katika wilaya za Ngorongoro na Arusha na hivyo kumtaka mfanyabiashara huyo tajiri wa tatu nchini Uingereza kusambaa zaidi katika wilaya nyingine nchini.

Aidha, amewataka walimu wakuu wa shule zote za msingi za serikali mkoani hapa kuwa waunganishi kati yao na serikali katika kutatua kero za walimu na kuboresha elimu kwa faida ya Watanzania wote.

Daqarro alisema hayo jana kabla ya kukabidhi vyeti vya walimu wakuu 25 wa shule za msingi za serikali waliohudhuria kozi ya mafunzo ya uongozi ya miezi sita iliyoandaliwa na Taasisi ya The Robbin & Sylvia Goodall Foundation inayoongozwa na tajiri huyo wa Uingereza.

Daqarro alisema serikali inamhakikishia ushirikiano mkubwa katika kuboresha elimu nchini ili kuendesha mafunzo ya kozi ya uongozi, kuzifanyia ukarabati shule za msingi na kujenga maabara za kisasa kwa ajili ya wanafunzi Naye Goodall aliyeambatana na mama yake mzazi Sylvia, alisema uamuzi wa kuwekeza katika elimu nchini ni mapenzi yake na wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa Watanzania.

Alisema Tanzania ina rasilimali nyingi sana na inatakiwa kuwa nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa na uchumi mkubwa na imara hivyo ameamua kutumia kozi hiyo kuelimisha walimu na wanafunzi kufahamu umuhimu wa rasilimali za nchi na kuzitunza.

Alisema elimu bora ndio msingi mkubwa katika kutunza rasilimali, hivyo basi taasisi yake imejikita kuboresha elimu ili watu wafahamu umuhimu wa rasilimali na kuzitunza. Goodall alisema alisikitishwa pale alipoona wanafunzi wanasoma kwa kukaa chini, chakula cha shida shuleni, umbali mrefu kutoka shule hadi nyumbani na ndio maana ameamua kutoa msaada wa madawati na kuzifanyia ukarabati shule zilizokuwa katika hali mbaya.

Mwaka huu, taasisi yake imepanga kutumia Sh biloni tatu kwa kazi hiyo. 
Awali, mkuu wa wilaya alisema kero zilizoko mashuleni zinapaswa kutatuliwa na pande zote mbili za walimu wakuu kwa kushirikiana na serikali ili wanafunzi wapate elimu bora na kuiachia serikali pekee ni kuionea.
Aliwataka walimu wakuu kutumia kozi hiyo kubadilika na kufanya kazi kwa weledi na kuacha kuwa na urasimu usiokuwa na tija. Daqarro alisema hakuna mwalimu mkuu aliyechaguliwa kufundisha kijiji na mwingine kufundisha mjini tu hilo halitawezekana na aliwataka walimu wakuu kubadilika kwa hilo na kuwataka kufanya kazi eneo lolote liwe la kijiji au mjini.

Naye Ofisa Elimu Taaluma na Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Ngorongoro, Anyamisye Mahali alisema mafunzo hayo yanaweza kubadilisha ufundishaji katika shule za msingi na wanafunzi kuwa na uelewa mpana kwa faida yao ya baadaye.

Post a Comment

0 Comments