Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata kumi na moja Halmashauri ya
Arusha wilayani Arumeru wamepatiwa msaada wa biskeli 11 na makabati 11
kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Johs Snow Ink 'JSI' Kanda ya
Kaskazini na kati linalojishughulisha na masuala ya Ulinzi na Usalama wa
mtoto.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitendea kazi hivyo Mkurugenzi wa JSI
ndugu Antony Mwendabaka amesema kuwa shirika limefikia uamuzi huo baada
ya kuona changamoto ya usafiri na utunzaji kwa kumbukumbu unaowakabili
watendaji hao katika kutekeleza majukumu yao kwa kulinganisha na
Jiografia ya maeneo yao.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia