Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWENYE MAFUNZO MBALIMBALI ILI KUJIAJIRI






Na Woinde Shizza,  Arusha
Wadau wa Ujasiriamali mkoani Arusha wametakiwa kutoa ushirikiano sanjari na kujitokeza katika mafunzo mbali mbali ya kada hiyo lengo likiwa kufikia adhma ya serikali kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mkurugenzi wa kampuni ya Zebra Promotion Zuberi Mwinyi alisema kuwa kama wajasirimali hawatakuwa na ushirikiano na kutoa nafasi kwa yale wanayojifunza kuwapa wenzao lengo la serikali halitafikiwa.
Amesema kuwa ili elimu ya ujasiriamali iwafikie watanzania kwenye maeneo mbali mbali nchini inahitajika nguvu ya ziada ambayo kila mmoja ashiriki kwa yale aliyonayo kuyatoa kwa lengo la kuboresha uzalishaji na kipato kwa wajasiriamali.
Amesema kuwa serikali imeandaa maeneo ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo na vya kati kwa lengo la vijana wa kike na kiume sanjari na wenye ulemevu kujitokeza kuanzisha viwanda na kuachana na dhana ya kuajiriwa ili waweze kujiajiri kufikia uchumi wa kati wa viwanda na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo.
“Ndio maana kampuni ya Zebra Promotion imekuja na mafunzo kwa kila kata kwenye mkoa wetu lengo likiwa ni kuwafikia vijana na kina mama hususani wauza mboga mboga na matunda kwa kuwapa elimu ya teknolojia ya kubadilisha mifumo ya maisha yao kwa kuwapa elimu ya uzalisha,uchakataji wa bidhaa na utunzaji wa fedha na mitaji” alisema Mwinyi.
Amesema kuwa masomo wanayotarajia kuyafundisha yamelenga kuwainua wajasiriamali wadogo kwenye kata zao na kuanzia tarehe 24 mwezi huu wataanza na Kata ya Ngarenaro kwa awamu ya pili baada ya awali kuwa na semina kama hizo katika kata mbali mbali za jiji la arusha ambazo zilileta tija na kuonyesha mwanga kwa kuinua vipato vya kinamama na vijana kwenye kata zao
Alisema kuwa kampuni yao imeendelea kufundisha uchakataji wa bidhaa za sabuni,shampoo,pinatbata mafuta mbali mbali.utengenezaji wa maandazi,ubuyu na keki, mishumaa.ufugaji bora wa kuku wa mayai na nyama na sungura,kilimo cha uyoga,sanjari kilimo cha mboga mboga kupitia kilomo nyumba(GREEN HOUSE) .
Amesema kuwa semina hizo za uzalishaji na kuwatafutia masoko na mitaji zinalenga kuwabaidilishi maisha kupitia sekta mbalimbali hapa nchini kwa kuwawezesha kuwapa elimu ya kukuza mitaji kwa kupitia vikundi vyao vya vicoba ili kuweza kukopesheka katika taasisi za kifedha hapa nchini.
Amesema kwa kushirikiana na Taasisi ya Kaizen kutoka nchini Japan na Sido watatembelea wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vikubwa mkoani hapa kutoa elimu na kuitangaza teknolojia ya Kaizen ili kuweka maboresho kwenye viwanda vyao ikiwemo mipangilio ya viwandani itakayoleta tija katika uzalishaji wao.

Post a Comment

0 Comments