siku niliyomtembelea Mutombo Lufungula Odax nyumbani kwake Rombo
ALIYETUNGA KIBAO CHA `MPENZI RUTA`
ATUMA SALAMU KWA BABU SEYA.
Mmoja wa wanamuzi mahiri na wa siku nyingi nchini ambaye pia ni mtunzi wa nyimbo ya Mpenzir Ruta ,Mzee Mutombo Lufungula Odax ambaye kwasasa yupo mkoani Kilimanjaro ,ametuma salamu za pole kwa mwanamuziki mwenzake ambaye walishirikiana naye kuimba pamoja katika bendi ya Gabijazzy kabla ya kubadilishwa na kuitwa Marquiz du Zaire.
Mzee Odax, akiongea nyumbani kwa mtoto wake katika wilaya ya Rombo, alisema kuwa anasikitishwa na kitendo cha Babu Seya na watoto wake kukumbwa na matatizo hayo na kwamba anamuombea kwa Mungu aweze kufarikjika na kutoka kwa msamaha wa Rais.
Odax alisema kuwa kibao cha Mpenzi Ruta ambacho alikitunga mahsusi kwajili ya mpenzi wake alishirikiana kuimba na waimbaji mbalimbali akiwamo Babu Seya ambaye alishiriki katika uimbaji na kusherehesha kwa gitaa nyimbo hiyo kiasi cha kupendwa na nchini na hata nje ya Tanzania .
Alisema kwamba anamkumbuka Babu Seya hasa katika umahiri wake katika nyimbo na maudhui ya nyimbo alizoimba na kushirikiana katika utunzi na Babu Seya ni pamoja nyimbo iitwayo 'Seya ya Mwivalo' ambaye alimtungia mwanamke mmoja jiji Dar es salaam.
Alisema kuwa uwanja wa muziki nchini Tanzania imepata pigo kwa masahibu yalimkuta mwanamuzi huyo mkongwe na kuwataka watanzania kuombea ili aweze kuachiwa kwa msamaha wa Rais na kwamba bado anamkumbuka na kumpa pole.
``Namkumbuka sana Babu Seya kwa kuwa tulikuwa naye katika bendi moja na tulishirikiana katika kila jambo na hasa katika nyimbo ya Seya wa Mwivalo ambaye tuliimba naye kwa umahiri mkubwa na hata katika vibao nvingine tulishirikaiana vizuri ``Alisema Mzee Odax.
Alisema kuwa neno liitwalo `Seya wa Mwivalo`linamaanisha msichana ambaye alipaswa kuwa mpenzi wa Babu Seya na walitunga nyimbo hiyo wakiwa vijana katika kikundi cha Skauti. Alisema Nyimbo hiyo iliyotungwa katika ya miaka ya 1984 na 1986 ilibeba ujumbe wa kweli na kwamba kila anapousikiliza anamkumbuka Babu Seya .
Amesema kibao chake cha 'Mpenzi Ruta' alishirikana kuimba na Babu Seya, Kasaloo Kyanga, Farashi Bukumbule na Kiniki Kieto.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia