KARIBUNI SANA WADAU KATIKA BLOG YETU YA LIBENEKE LA KASKAZINI, TUMA MAONI NA MATANGAZO YAKO AU TUPIGIE SIMU NAMBA +255 755 264 620 KARIBU SANA....

Monday, October 24, 2016

MAHAKAMA YA RUFAA YASHIDWA KUTOA UKUMU KESI YA UCHAGUZI INAYOWAKIBILI ONESMO NANGOLE NA DKT KIRUSWA

mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiongea na waandishi wa habari mara baada ya  maamuzi ya ruf
aa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la longine Onesmo Nangole
Na Woinde Shizza,Arusha 

Mahakama ya rufaa kanda ya Arusha imeshindwa kutoa maamuzi ya rufaa iliyofunguliwa  na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido ,Onesmo Nangole(CHADEMA) ambaye anapinga maamuzi ya mahakama kuu iliyomvua ubunge wake, badala yake imeagiza mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo aunganishwe katika shauri hilo.

Aidha mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa mrufani kwa ajili ya kufanya marekebisho ya notisi yake ya rufaa na kuyaleta mahakamani hapo ili msimamizi wa uchaguzi pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali waingizwe  kama mashaidi  muhimu katika rufaa.

Akisoma taarifa ya majaji watatu walikuwa wakisikiliza rufaa hiyo mahakamani hapo Msajili wa mahakama rufaa John Kayanza alisema kuwa mahakama ya rufaa aitatenda haki katika hukumu yake iwapo haita msikiliza mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Longido na imewataja kama mashaidi muhimu kwa upande wa mrufani

“kama mahakama itatoa uamuzi bila kusikiliza mwanasheria wa serikali na msimamizi wa uchaguzi haitakuwa imetenda haki  katika mahamuzi hivyo mahakama imeonelea ni vizuri  mrifani akaifanyie marekebisho notisi yake na ndani ya siku 21 aiwasilishe mahakamani”alisema Kayanza

Katika rufaa hiyo mrufani Onesmo Nangole aliyekuwa mbunge wa jimbo la Longido alikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo ilitengua ubunge wake na kuagiza msimamizi  wa uchaguzi atangaze jimbo hilo kuwa lipo wazi.

Katika kesi hiyo Onesmo Nangole( CHADEMA) anawakilishwa na mawakili wawili ambao ni  Methodi kimomogoro akisaidia na wakili John Materu ambapo kwa upande wa warufaniwa Dkt.Steven Kiruswa (CCM) anawakilishwa na mawakili watatu wakiongozwa na DKT.Masumbuko Lamwai akisaidiwa na Daudi Haraka pamoja na Edmond Ngemela.

Rufaa  hiyo inasikilizwa  na Majaji  watatu ambao ni jaji Sauda   Mjasiri,Jaji Musa Kipenka pamoja na Profesa Ibrahimu Juma.

Akiongea mara baada ya kesi hiyo kuairishwa Onesmo Nangole alisema kuwa anaishukuru mahakama kwa kuwapa nafasi na kuona umuimu wa mwanasheria wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wilayani longodo kuja kutoa ushaidi katika shauri hilo na anaamini mahakama hiyo itamtendea haki.


Kwa upande wa Dkt,Kiruswa (CCM) alisema yeye atatizo na maamuzi ya mahakama na anaiachia mahakama iendelee kushulikia shauri hilo na anaamini itatenda haki.
soma zaidi...

WATANZANIA WAASWA KUITUNZA NA KUOMBEA AMANI YA NCHI


 Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa   akizungumza na waandishi wa habari mara baada tu ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha


 Umati wa wakazi wa 
mkoa wa Arusha waliofurika katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Kilimanjaro(KIA) kumpokea Nabii B.G Malisa ambaye atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini A
rusha

Na Woinde Shizza,Arusha
 Watanzania wametakiwa kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya machafuko. 


Wito huo umetolewa jana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Ukombozi hapa nchini, Nabii B. G Malisa wakati alipokuwa akihubiri neno la Mungu katika viwanja vya reli jijini Arusha. Nabii Malisa alisema kwamba watanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanaombea amani ya nchi inaendelea kutawala hapa nchini.Alisema ya kwamba amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika nchi mbalimbali duniani na kushuhudia hali ya usalama ikiwa tete ambapo askari wamekuwa wakitembea mitaani huku wameshika silaha za moto. "Hivi karibuni nilikuwa Nigeria wakati nashuka uwanja wa ndege nilipokelewa na askari wenye silaha za moto nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu amani tuliyonayo hapa Tanzania "alisema Malisa Hatahivyo, alitoa wito kwa serikali kuunga mkono juhudi za viongozi mbalimbali wa dini hapa nchini katika kuwasaidia vijana na kusema viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa katika kuwainua watu kiuchumi na kuwaepusha na vitendo viovu. Awali akizungumza na waandishi wa habari mchungaji wa kanisa la Ukombozi tawi la Arusha Mchungaji Ushindi alisema kwamba mhubiri huyo atakwenda kufanya huduma ya maombezi mkoani Arusha kwa siku nane na kuwataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi

soma zaidi...

UVCCM YATOA SIKU SABA MAALIM SEIF AZUILIWEKUENEZA SIASA MSIKITINI

kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka
Na Woinde Shizza, Dar es  salaam.
Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi umetoa siku saba kwa serikali  ya Mapinduzi Zanzibar  (SMZ ) kuchukua hatua sahihi dhidi ya wanasiasa wanaohubiri siasa kwenye nyumba za ibada vingingevyo UVCCM nayo itaingia mitaani kuuthubitishia ulimwengu kuwa hakuna utii  wala utawala wa sheria visiwani humo.
Umoja huo pia umemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwiguli Nchemba, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Zanzibar Mohd Aboud  na msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kutoka hadharani na kuthibitisha iwapo  kinachofanywa hivi  sasa  na Katibu Mkuu wa CUF  Seif sharif Hamad ni matakwa ya sheria vyama vingi No 5 ya mwaka 1992.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo jana alipoongea na waandishi wa habari kufuatilia kauli ya uvccm waliyoitoa hivi karibuni kutahadharisha  juu ya  kitendo cha Maalim Seif kuendelea kuhutubia siasa kwenye nyumba za ibada visiwani humo  huku mamlaka za dola zikiwa kimya na kushindwa kumdhibiti kwa mujibu wa Katiba  na sheria .
Shaka alisema ni mambo ya ajabu sana kumuona mwanasiasa mmoja  akiendelea kuzitumia nyumba za ibada kueneza siasa za chuki bila kuchukuliwa hatua za kisheria huku akitamba mitaani kama kwamba Nchi haina sheria, Katiba wala viongozi dhamana.
"Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais na Msajili wa Vyama Vya Siasa sasa watoke hadharani ili  kuthibitisha iwapo yanayofanywa na Maalim Seif ni matakwa ya sheria ya vyama vingi au ni ubabe wa kisiasa"alieleza Shaka.
Alisema imefika mahali Vijana   hawaelewi kama yupo mwanasiasa ambaye aliye  juu sheria na Katiba hadi afikie kubeza  sheria na taratibu za Nchi bila kuchukukiwa hatua stahiki 
Shaka alisema UVCCM imefika mahali haijui kama yupo  kambare au hongwe, tujuavyo hakuna ushirika katika kuendesha ufalme, ufalme ni mmoja na kila raia anapaswa kuheshimu sheria na vyombo vya dola.
Aidha alieleza kuwa hakuna mtu aliyemshawishi Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif  akilazimishe chama chake kisusie uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu hivyo anapohamishia siasa kwenye nyumba za ibada ni wazi sasa ana mpango hatari wa kuiingiza nchi katika ghasia na machafuko.
"Hivi ni nani Maalim Seif Zanzibar , yeye ana mamlaka yepi hadi akaidi sheria za nchi huku akitazamwa macho , kwa nini anatamba na kufanya atakavyo, viko wapi vyombo vya ulinzi na usalama, wasipotoa majibu muafaka  tutaingia mitaani ili kuyahami Mapinduzi yetu "alisema Kaimu huyo..
Alieleza kuwa Mapinduzi ya januari 12 mwaka 1964 yalioleta manufaa   kwa kizazi cha wakwezi na wakulima  baada ya miaka 50 kupita, haya ni Mapinduzi ya  vijana, yalifanywa na vijana wenzetu na sasa tutayatea   wala si Mapinduzi ya kuchezewa na wasaliti au vibaraka , tutampima kila kiongozi kwa ujasiri au usaliti wake .
Shaka alisema Maalim Seif alihutubia msikitini huko Mbuyuni, akaenda Khinani pia ijumaa iliopita  amehutubia msikiti wa kwa Bi Zired bila vyombo vya ulinzi na usalama wa raia kumchukukulia hatua zozote huku mwanasiasa huyo na wafuasi wake wakijigamba mitaani .
"Uvccm tunaheshimu dhana ya utawala wa sheria ila si washindwa wa kuleta ghasia popote pale, ikiwa waliopewa dhamana za juu wanajivika macho yenye makengeza , hatutasita kuingia barabarani wakati wowote na hapo dunia isije ikatulaumu "alisema shaka
Juhudi za kumpata katibu mkuu wa cuf Maalim Seif , Waziri Mwigulu Nchemba na Mohamed Aboud ziligonga ukuta baada ya simu zao kuita muda mrefu 
bila kupokelewa hadi tukienda mitamboni
soma zaidi...

DC LONGIDO,DANIEL CHONGOLO AMSWEKA NDANI MKANDARASI WA BARABARA

DC-Longido,Mh Chongolo.
Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Godfrey Chongolo amemtia ndani Mkandarasi anayejenga barabara ya Longido-Kitumbeine-Oldonyolengai Bw. Loserian Sokonei Mollel kutokana na uzembe na kutotimiza matakwa ya mkataba na kuwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo pamoja  na wananchi kwa ujumla. 

Mkandarasi huyo anayemiliki kampuni ya Genuine Company Limited amekuwa akiendesha shughuli za ujenzi wa drift katika barabara hiyo bila kutengeneza barabara mchepuko (diversion) katika maeneo hayo na kusababisha mara kwa mara wasafiri kukwama na kulala porini. 

Wakizungumza na mtandao huu, wananchi wa kijiji cha Gelai Lumbwa wamepongeza uamuzi wa DC Chongolo kwa sababu unasaidia kuondosha na kutatua kero zanazowasumbua na kuwakwaza kwenye maisha yao ya kila siku. "Tulichoshwa na watu waliokuwa wakifanya mambo vile wanavyotaka wao. Kwa hakika hii ni awamu ya Kazi Tu, tunamshukuru DC na OCD na tunamuunga mkono" alisema Mesiaki Laizer.
soma zaidi...

WILAYA YA HAI WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Juliet Mushi akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzo wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Baadhi ya wananchi wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi.
Msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi ukiwa umechimbwa na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule zilizoko wilaya ya Hai.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza wakati akizindua rasmi kampeni za kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi juu ya wazo la kuanzishwa kwa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakinyanyua mikono kuashiria kuunga mkono kampeni hiyo.
Diwani wa kata ya Masama Kusini Elingaya Masawe (Chadema) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari wilayani Hai.
Diwani wa kata ya Bomang'ombe ,Joe Nkya (Chadema) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa uliofanyika katika shule ya msingi Msamadi wilayani Hai.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Diwani wa kata ya Machame Magharibi Goodluck Kimaro (Chadema) akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya akizungumza namna wanavyoshirikiana na Madiwani wa upinzani katika shughuli za menedeleoo ya wananchi wilayani Hai.kulia kwake ni Diwani wa kata ya Masama Mashariki ,John Munis (Chadema).

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa maelezo juu ya namna wananchi watakavyo changia katika ujenzi wa madarasa kwa njia ya harambee ili kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchhi waliofika katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wakitoa ahadi zao wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo katika kijiji cha kwa sadala.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo kijiji cha Kwa Sadala wilayani Hai.
Mafundi ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa mara baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo Swissport wametoa kiasi cha Sh Mil 15. 

soma zaidi...

SHAMBA LA MITI LUNGUZA WAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI MUHEZA WAKABIDHI MADAWATI 200


Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akipokea madawati 200 kutoka kwa Meneja wa Shamba la Miti Lunguza, yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Abdallah Mchomvu katika halfa iliyofanyika leo

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akikagua madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akitazama baadhi ya madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Meneja wa Shamba la Miti Lunguza,Abdallah Mchomvu akizungumza katika halfa hiyo ya kukabidhi madawati kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kushoto aliyekaa ambayo yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)
 Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza ambaye ni Afisa Tarafa ya Muheza Khatibu Omari wakati wa halfa hiyo wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Lunguza ambalo ni la serikali linalojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na ustawishaji wa miti ya misaji (Teak)
Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya MuhezaHajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo.
soma zaidi...

HUDUMA YA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA YAFANA MKOANI DODOMA.

Huduma ya injili iliyofanywa na mchungaji kiongozi wa Kanisa la "EAGT Lumala Mpya Internationa Church " lililopo Sabsaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), mkoani Dodoma imekuwa ya kufaana na watu wengi wameokoka na kubarikiwa.

Ni katika mkutano wa injili ulioandaliwa na kanisa la Siloam EAGT Ipagala mkoani Dodoma kwa juma zima ambapo unatariwa kufikia tamati kesho Oktoba 23, 2016.
Picha na Jorum Samwel
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akiendelea na huduma ya maombezi mkoani Dodoma
Wengi waliponywa na wanaendelea kuponywa kwa jina la Yesu, vifungo vilivyowatesa kwa muda mrefu.
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akifanya maombezi mkoani Dodoma.
soma zaidi...

Google+ Followers

 
Copyright ©2010-2014 LIBENEKE LA KASKAZINI • All Rights Reserved.
Template Design by Gadiola Emanuel • Powered by Blogger
back to top