Mkurugenzi wa taasisi ya Zaina Foundation Zaituni Njovu akiendelea kutoa mafunzo juu ya matumizi ya teknolojia Kwa wa wanawake wa Kijiji cha Kilomo kata ya Kilomo wilaya ya Bagamoyo .
Katika kuelekea katika kilele cha siku ya wanawake Duniani taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Zaina Foundation imetoa elimu ya matumizi sahihi ya teknolojia pamoja na namna gani teknolojia inaweza kumkwamua mwanamke wa kijijini kiuchumi Kwa zaidi ya wanawake 30 waishio katika Kijiji cha Kilomo kata ya Kilomo wilayani Bagamoyo
Akiongea katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa taasisi hiyo Zaituni Njovu alisema kuwa katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake waliona ni vyema kwenda katika Kijiji hicho kuwapatia wanawake elimu ya kutambua ninamna gani wanaweza kutumia simu zao za mkononi (smart phone)kuweza kujipatia masoko ,kuweza kujipatia wateja wapya na pia kuweza kujenga uaminifu Kwa wateja wao.
Aidha pia alisema kuwa wameweza kuwaelimisha juu ya ukatili wa kijinsia ambao unafanyika mtandaoni Kwa wanawake ambapo pia alibainisha kuwa hata wanawake wa Kijijini pia ni wahanga katika tatizo hilo .
"Kulingana na kauli mbili yetu ya siku ya wanawake ya mwaka huu 2024 ambayo inasema Wekeza kwa Wanawake katika Teknolojia (Haki za Kidijitali) ili Kuharakisha Maendeleo katika Uhuru wa Kiuchumi , kulingana na kauli mbiu hii ndio maana tukaamua kuchagua hawa wa kijijini tuweze kuwawezesha kwenye eneo hili la matumizi sahihi ya teknolojia , namna gani wanapata fursa zilizopo katika teknolojia,namna gani wanaweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yapo uko mtandaoni ikiwemo wizi wa mtandaoni na kuweza kuibiwa taarifa zako na mtu mungine kupitia teknolojia "alisema Zaituni