WATANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

 

Na Woinde shizza ARUSHA 


Watanzania wametakiwa kuwekeza nguvu zaidi katika kufanya kazi Kwa bidii haswa katika kipindi hichi ambacho dunia imeyumba kiuchumi Ili waweze kusonga mbele kimaisha .

Hayo yameelezwa na mwalimu wa neno la Mungu ambaye pia ni mtaalam wa uchumi Mgisa Mtebe wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya uchumi Kwa waumini wakanisa la Angalican parish ya St.Jemsi Arusha lililopo katika dayosisi ya Mount Kilimanjaro wakati wa hitimisho la kongamano la pasaka la siku Kumililifanyika kanisani apo ambapo alisema kongamano hilo litakuwa likifanyika Kila mwaka.


Alisema kuwa kongamano hilo limebeba ujumbe usemao uwezo wa damu ya Yesu kukomboa uchumi wa Mtu mmoja Moja ambapo alifafanua kuwa somo hili linamfundisha mwananchi ni namna gani ataweza kuinua uchumi wake wa kimwili na kiroho kupitia damu ya Yesu

Alisema kuwa wakati dunia imeingia katika mtikisiko mkubwa sehemu mbalimbali ikiwemo nchi yetu vitu vimepanda bei , hali ya maisha imezidi kuwa juu , magonjwa mbalimbali kuibuka Pamoja na dhiki kuu kutawala ni muda muhafaka wa Kila mwananchi kufanya kazi Kwa bidii huku akiendelea kumuomba Mungu 

"Dhana ya uchumi Mungu alipoanza uumbaji alipomuumba adamu alimpa Mamlaka ya kumiliki vitu vyote vilivyopo nchini hivyo ,unapotawala nchi na rasilimali zake unatakiwa uwe na moyo wa utulivu ,kazi ya damu ya Yesu kutufundisha namna ya kumiliki vya kidunia pamoja na kumiliki vya ki Mungu"alisema Mtebe

Alisema uchumi wa dunia makadirio yake yanategemeana na wakati uliopo pindi mabadiliko tu yanapotokea basi Kwa namna yeyote Ile lazima uchumi uyumbe na kutokana naagonjwa mbalimbali yaliyoibuka pamoja na vita katika nchi za wenzetu ndio zimepelekea uchumi kuyumba na vitu kupanda pamoja na maisha kubadilika.

Allibainisha kuwa ni vyema wananchi wanaposherekea pasaka wakaweka imani katika kristo Yesu aliefufuka ,ni vyema wakawe watu wa imani pia wamuhisishe sana Mungu katika kazi zetu pamoja na kuwa watu wenye maadili mema.


Kwa upande wake mmoja wa muhumini wa kanisa hilo Meshack Mtweve alisema kuwa semina hiyo itamewasaidia kujua mambo mbalimbali ya kiuchumi na anaamini baada ya semina hiyo atabaki kama alivyo kwani ata lia tena.

"Dunia inapita katika mtikisiko wakati dunia inalia wanawa mungu hatutakiwi kulia tena maana tuna damu ya Yesu iliotishindia "alisema Mtweve.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post