BREAKING NEWS

Monday, April 4, 2022

CAMARTEC YABUNI MASHINE YA KUOTESHEA PAMBA KWA WAKULIMA.

 

Kaimu Meneja uzalishaji kutoka Camartec ,Injinia Boniface Massawe akizungumzia kuhusiana na jiko hilo la kisasa linalotumia mwanga wa jua (Sola),Happy Lazaro.
************************

Arusha.Kituo cha Zana za  kilimo na Teknolojia vijijini (Camartec) imebuni  mashine maalumu kwa ajili ya kupandia  pamba ambayo ina uwezo wa  kuotesha sehemu kubwa kwa muda mchache.
Hayo yalisemwa  na Kaimu  Meneja uzalishaji kutoka Camartec Injinia Boniface Massawe wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na watafiti waliotembelea kituo hicho  kujionea shughuli zao ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo yaliyotolewa na Tume ya  Taifa ya sayansi na Teknolojia  (COSTECH).
Injinia Massawe amesema kuwa,wamebuni mashine hiyo maalumu kwa ajili ya kupandia pamba ambayo itawarahisishia wakulima kuweza kupanda zao hilo  ndani ya muda mfupi .
“mashine hii ina uwezo wa kupanda pamba kwenye shamba la heka moja ndani ya muda mfupi na kuweza kuokoa muda ambao wakulima wangeweza kuutumia kukaa muda mrefu shambani kwa ajili ya shughuli hiyo “amesema Massawe.
Aidha ameongeza kuwa,wamefikia hatua ya kuja na mashine hiyo kwa lengo la kuweza kuwarahisishia wakulima wa zao hilo kulima kisasa zaidi na kuweza kupanda zao hilo kwa kutumia njia za kisasa kupitia mashine hiyo.
Hata hivyo amewataka wakulima kujitokeza kwa wingi kutumia mashine hiyo kwani itawasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa muda wa kukaa shambani na kuweza kufanya shughuli zingine.
Hata hiyo amesema kuwa ,mbali na mashine hiyo ya kuotesha pamba pia wameweza kubuni jiko maalumu la kupikia linalotumia mwanga wa jua (Sola) ambalo linasaidia  kutunza mazingira na lina uwezo mkubwa wa kupika chakula ndani ya muda mchache na kuokoa gharama.
Massawe amesema kuwa, wamefikia hatua ya kuja na jiko hilo kama njia mojawapo ya utunzaji wa mazingira kwani jiko hilo linatumia nishati ya jua pekee na halina gharama yoyote tofauti na majiko mengine.
Amesema kuwa, jiko hilo lina uwezo wa kupika chakula ndani ya dakika 49  ambapo linafaa kupikia vyakula kama nyama, kuchemsha maharage,makande ambapo limekuwa likinunuliwa na wateja wengi kutokana na kutumia muda mchache kupika na kuokoa muda.
“Jiko hili linapatikana kwa gharama ya Shs 600,000 tu na wateja wengi wanayanunua baada ya kuona mafanikio yake kwani wengi wao wanaotumia ni wafanyabiashara ambao wanajikuta wakipika vyakula vingi ndani ya muda mchache huku wakiokoa gharama za matumizi mengine”amesema.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates