BREAKING NEWS

Thursday, April 21, 2022

WATENDAJI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO

 


Na Fatma Ally , Dar es Salaam



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija amewagiza  watendaji wa Halmashauri ya Jiji wote kutoa ushirikiano na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala katika Utekelezaji wa  majukumu yao ya kazi


Agizo hilo, amelitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizindua  kampeni ya upandaji miti 5000 iliyondaliwa na jumuiya ya wazazi Wilaya ya Ilala iliofanyika  Shule ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi Tabata Kimanga.


"Kukua kwa CCM kwa ajili ya Jumuiya, Jumuiya ya Wazazi ina jukumu kubwa sana naagiza kwa Watendaji wa Kata na Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Jumuiya ya Wazazi kwani Jumuiya ya Wazazi ni Mzizi wa Malezi ya Familia" amesema Ludigija.



Aidha,amesema licha ya kuzindua miti 5000 iliyotolewa na wakala wa misitu (TFS) lakini  mpango mkakati wa Wilaya hiyo ni kupanda miti mill 1.5 ambapo mwaka Jana walipanda miti 75000. 


Akizungumzia suala la  malezi ya familia, amesema yananzia ngazi ya Kata na mitaa hivyo Jumuiya hiyo ina jukumu kubwa sana kushirikiana na Watendaji wa Serikali katika kufatilia Maendeleo ya watoto ikiwemo shule.



Hata hivyo, amempongeza Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe na Katibu wake kwa tukio hilo kubwa na la kihistoria walilolifanya la kuanzisha kampeni hiyo kwani itasaidia kuboresha mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


"Mabadiliko ya tabianchi yana athiri nchi yetu kwa kiasi kikubwa kutokana na uharibifu wa Mazingira, mkaa ni zao la misitu na Dar es Salaam ni watumiaji wakubwa wa rasilimali ya misitu, hivyo upandaji wa misitu hii utasaidia kwa kiasi kikubwa "amesema Ludigija. .



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Ilala, Mohamed Msophe amesema miti hiyo 5000 ni kampeni ya Ilala ya kijani ambapo itasambazwa kila kata miti 20 ,ngazi ya matawi miti 15, Ili kuhakikisha kila kaya inapanda miti hiyo kwa kupitia matawi yote 265 ya Jumuiya ya wazazi.


Aidha, amewataka viongozi wake wa Jumuiya hiyo kupanda miti hiyo Shuleni, katika vituo vya Afya na Ofisi Serikali, huku akibainisha kuwa kamati ya Utekelezaji wilaya itakuwa inafanya ziara kufatilia Maendeleo yake mpaka inakuwa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates