Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella akiongea na waandishi juu ya uzinduzi wa filamu maarufu ya Royal Tour
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu anatarajiwa kuwasili jijini Arusha April 28 Kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa filamu maarufu ijulikanayo kama Royal Tour inayotangaza vivutio mbalimbali vya utalii
Akiongea na waandishi wa habari mapema Leo mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amesema kuwa Rais anatarajiwa kuja kuzindua rasmi filamu hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini tangu ilipozinduliwa rasmi nchini Marekani April 18 na baadae aprili 21 katika jiji la Los Angeles nchini Marekani
Alisema kuwa filamu hiyo itasaidia kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo apa nchi ambapo pia utasaidia kuvuta wawekezaji wengi zaidi ,pamoja na kuvutia watalii wengi "
Mongella alisema kuwa uzinduzi wa filamu hiyo utatochea utalii Kwa kiwango kikubwa sana hivyo Wananchi na wadau wa sekta ya utalii wanatakiwa kuunga mkono ujio huo Kwa kuwa una manufaa makubwa sana
Alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano (AICC)ambapo Kwa Arusha ni kitovu Cha utalii na hiyo ni nafasi pekee na ya heshima
Alifafanua kuwa uzinduzi huo unatarajiwa kuwa na wageni na viongozi mbalimbali wa kitaifa,mabalozi,wawekezaji,wadau wa utalii na Uhifadhi, wafanyabiashara,pamoja na Wananchi kutoka katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
"Kwa sasa nchi yetu idadi ya wataliiwa ndani wanaotembelea maeneo ya Hifadhi imeongezeka kutoka wastani wa watalii 562,549 mwaka 2020 hadi watalii 788,933mwaka 2021halikadhalika watalii620,867 mwaka 2020 hadi kufikia watalii 922,692 mwaka2021"alisema Mongella
Alisema kuwa kupitia juhudi za Rais kama muongoza watalii namba Moja (Tour Guide)
Katika utengenezaji wa filamu hii itaendelea kuongeza chachu na muitikio mkubwa zaidi Kwa wageni watakaotembelea nchi yetu
Alisema tangu kuanza kurekodiwa filamu hii kumekuwa na ongezeko ya watalii na hii imeshuhudiwa haya wiki Moja iliopita nchi yetu ilipokea kundi kubwa la watalii kutoka nchi ya Israel.
"Mtakumbuka kuwa maeneo ya kaskazini ambapo filamu hii ilirekodiwa ni pamoja na Hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro ,Vivutio vya utalii vilivyopo katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro , Hifadhi ya taifa ya Serengeti pamoja na eneo la uzalishaji wa Tanzanite lililopo Mererani"alisema Mongella
Alitoa rai na kuhamasisha Wananchi hasa WA mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kujitokeza Kwa wingi katika maeneo yaliyoainishwa katika barabara zetu Kwa ajili ya kumpokea Rais na ujumbe wake kuelekea uzinduzi huo wa filamu hiyo ya Royal Tour.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia