Waziri Bashungwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Kaidi

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Innocent Bashungwa  amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Hassani Njama Hassani kuanzia leo tarehe 20.04.2022 ili kupisha uchunguzi.


Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya Tarehe 10.03.2022 Wilayani humo.


Wakati wa ziara hiyo Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa Fedha za miradi na matumizi yasiyo sahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, jiko na bweni na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi Wakuu wote wa Idara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo.


Hadi kufikia leo hii hakuna Mkuu wa Idara yeyote ama Mtumishi aliyechukuliwa hatua kufuatia maagizo hayo, aidha Waziri Bashungwa ameendelea kuwataka Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini ubadhifu wa fedha za umma.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post