Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA WAGENI 5000 KUHUDHURIA UZINDUZI WA FILAMU YA ROYAL TOUR ARUSHA

Takribani wageni 5,000 kutoka maeneo mbalimbali wanatarajia kuhudhuria katika uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour utakafanyika kesho mkoani Arusha ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.


Akizungumzia maandalizi ya uzinduzi huo leo Jumatano Aprili 27, 2022 Mwenyekiti wa kamati ya Taifa ya uzinduzi wa filamu hiyo, Dk Hassan Abbas amesema tayari maandalizi yamekamilika.



Dk Abbas amesema filamu hiyo itazinduliwa Arusha kesho na baadaye Zanzibar Mei 7 na uzinduzi rasmi utafaanyika Mei 8 jijini Dar es Saalam ambapo siku hiyo filamu yote n itarushwa yote moja kwa moja.


Amesema siku hiyo ya uzinduzi jijini Dar es Salaam ndipo filamu itatolewa kwa vyombo vyote vya habari na itakuwa bure kwa Watanzania wote.


Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema filamu hiyo licha kuzinduliwa nchini pia tayari imewekwa kwenye mtandao wa Amazon wenye watu zaidi milioni 150.


Amesema pia filamu hiyo tayari imeanza kutazamwa na runinga 350 za majimbo nchini Marekani ambapo watu zaidi ya million 130 wanatarajia kuona.


Sababu za Wamarekani kupewa tenda

“Ile filamu uzinduzi wake ni Tarehe Aprili 18 na utafanyika mara mbili New York na Los Angels, sasa mnauliza kwa nini walirekodi wageni na si Watanzania? Unachokifanya lazima uwe na malengo.


“Sisi malengo yetu kwenye filamu hii ni kuifikia dunia na kuiambia fursa zetu za utalii na uwekezaji na biashara, sasa rafiki yangu Ukimchukua Msigwa aende akarekodi hiyo filamu si ataishia kutazama Zungu

Post a Comment

0 Comments