Ticker

6/recent/ticker-posts

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA WADAU WA SEKTA YA KILIMO

 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),  Dkt. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 13, 2022 wakati akitoa uaanuzi juu ya athari zitakazojitokeza baada ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi na miumo ya hali ya hewa. Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),  Dkt. Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 13, 2022 wakati akitoa uaanuzi juu ya athari zitakazojitokeza baada ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi na miumo ya hali ya hewa. Kulia ni Mratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Usimamizi wa Maafa, Khawa Malageni.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ushauri  kwa wadau wa sekta za Kilimo, Usalama wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, Nishati na Maji, Mamlaka za Miji, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa kutokana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na miumo ya hali ya hewa.

Akizungumza leo Aprili 13, 2022 Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Dkt. Agnes Kijazi amesema kuwa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo uliohuishwa wa msimu wa mvua katika kipindi cha Machi hadi  Mei, 2022.

Amesema kuwa kumejitokeza mabadiliko ya muda mfupi ya joto la bahari katika eneo la pwani ya Afrika Mashariki na eneo la mashariki mwa bahari ya Hindi. Mabadiliko hayo ya muda mtupi ya joto la bahari ambayo ni nadra kutokea kutokana na tabia ya bahari kutunza joto au baridi kwa muda mrefu yamesabishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kuwa kumekuwepo na Vipindi virefu vya ukavu vilivyojitokeza katika kipindi cha Machi, 2022 hususani kwa maeneo ya pwani ya Kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki ambapo maeneo hayo yalipata mvua chache.

"Hali hiyo ya vipindi virefu vya ukavu imesababishwa na matukio ya vimbunga katika Bahari ya Hindi eneo la Rasi ya Msumbiji kusini zaidi mwa eneo ambalo lingesababisha vimbunga hivyo Kuongeza mvua katika maeneo ya nchi yetu." Amesema Dkt. Agnes

Amesema Mwenendo huo wa vimbunga na mabadiliko katika joto la bahari vimechangia Ukanda mvua kuendelea kusalia katika maeneo ya kusini mwa nchi ambapo kwa kawaida katika kipindi cha mwanzoni mwa Machi huanza kuelekea maeneo ya kaskazini mwa nchi. 

Hali hiyo imesababisha kuvurugika kwa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kuathiri mwenendo wa unyeshaji wa mvua za Masika kwa 2022.

 Athari zinazotarajiwa
ni pamona na Upungufu wa unyevunyevu katika udongo ambapo hali hii inaweza Kuathiri upatikaji wa mazao, upatikanaji wa maji na malisho kwa ajili ya mifugo na wanyamapori, upungufu wa kina cha maji katika mito, mabwawa na hifadhi ya maji ardhini.

Upo uwezekano wa kuongezeka kwa athari za magonjwa ya kuambukiza, hususani magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo salama kwa afya.

Vipindi virefu vya ukavu, milipuko ya wadudu dhurifu kwa mazao kunaweza kusababisha athari za kunyauka kwa mimea.

Shughuli za ujenzi, usafiri na usafirishaji zinatarajiwa kunufaika katika vipindi vya mvua chache.

Wakulima wanashauriwa kuzingatia matumizi ya mbinu na teknolojia za kilimo himilivu za kuhifadhi maji na unyevunyevu wa udongo pamoja na kuzingatia maelekezo ya maafisa ugani katika maeneo yao.

Jami inashauriwa kuweka mpango mzuri wa matumizi endelevu ya rasilimali za
maji na uhifadhi wa malisho.

 Mamlaka husika zinashauriwa kushirikiana na kuhakikisha uwepo wa usalama wa
chakula, malisho ya mifugo, maji na kutoa miongozo ya namna ya kukabiliana na hali ya upungufu wa mvua unaotarajiwa kujitokeza.

Akizungumza jinsi watakavyo kabiliana na mabadiliko hayo, mdau wa Kilimo, Juma Makali amesema kuwa watajiunza njia rahisi ambazo zitawasidia katika kukabiliana na changamoto ya maji pamoja na kuwashauri wakulima mbegu za mazao ambazo yatatumia muda mfupi kukomaa

Post a Comment

0 Comments