Mkurugenzi wa TEMDO Mhandisi Fredrick Kahimbaakionyes ha Moja ya mtambo ambao Taasisi hiyo unaitengeneza
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Wakulima wa zao la parachichi wameondokana na tatizo la kuharibika kwa zao hilo baada ya mavuno mara baada ya taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo (TEMDO)kuwaletea mtambo itakayo wasaidia kuchakata mafuta Kwa ajili ya kupikia pamoja na kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi.
Aidha pia mtambo huo pia utasaidia kupunguza idadi kubwa ya maparachichi ambayo yalikuwa yanashidwa kusafirishwa nje ya nchi kutokana na kutokuwa na ubora unaostaili.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka TEMDO Dkt. Sigsbert Mmasi alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakikabiliwa na upotevu wa parachichi ambao unatokana wingi pamoja na ubovu ambao unapelekea kuharibika katika kipindi cha msimu wake.
Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo TEMDO iliamua kufanya utafiti Kwa kuwatembelea wakulima wa zao hilo wa mikoa ya Kilimanjaro ,Iringa na Mbeya na kuangalia namna ya kuwasaidia kupunguza tatizo hilo ndipo wakaamua kutengeneza mashine ambayo itawasaidia kumaliza tatizo hilo kwa kubuni
mashine hiyo ambayo itawezesha wakulima kuepukana na upotevu wa maparachichi.
Alibainisha kuwa mashine hizo wanazitengeneza kwa ajili ya wajasiriamali wadogo , wakubwa na wakati ambapo ambapo itasaidia mkulima mwenyewe kuweza kuchakata parachichi hizo kwa mahitaji yake ya mafuta ya kupikia , mafuta Kwa ajili ya urembo pamoja na matumizi ya biashara.
"mashine hizi pia zitatumika kama shamba darasa ili kuwezesha wakulima kujifunza pamoja na kuwawezesha wajasirimali ambao wanauhitaji waweze kujifunza teknolojia hiyo
hadi sasa tumeshatembelea viwanda vikubwa vitatu vilivyoko Arumeru lengo likiwa ni kupata taarifa za kubuni teknolojia , ubunifu wa mashine hizi upo kwenye mchoro na natunatarajia hadi mwezi wa saba tutakuwa tumekamilisha utaratibu wa mashine hizo huku mwezi wa kumi na mbili tukitarajia kufanya majaribio ya mashine hizi"alisema Mmasi
Alisema kuwa mradi huu wa kutengeneza mitambo ya kukamulia mafuta ya parachichi kwa ajili ya wakulima wa zao hilo wameweza kupata ufadhi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH )ambapo imetoa kiasi cha shilingi shilingi milioni 117 kwa ajili ya mashine mbili ambapo mashine moja ni Kwa ajili ya kukamulia Mafuta ya parachichi ambalo yameiva na mtambo wa pili ni Kwa ajili ya ya kukamulia mafuta ya parachichi ambalo alijakomaa ambapo alibainisha kuwa mtambo huu wa pili utamuwezesha mkulima kuvuna parachichi lililokomaa na kulikamua bila kusubiri kuiva.
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo ya uandishi wa habari za kiutafiti kutoka Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia Dkt Baraka Msangi alisema kuwa tafiti hizi zikiandikwa vyema kwa lugha rahisi na zikawafikia wananchi itawasaidia kufanya maamuzi katika kutatua yao ya kila siku kama vile kuambua namna ya kuokoa maparachichi yao yaliokua yakipotea Kila mara.
Tags
HABARI MATUKIO