BREAKING NEWS

Saturday, April 2, 2022

YAJUE MAHARAGE BORA YALIYO NA MADINI YA CHUMA PAMOJA NA ZINKI

 


Na Woinde Shizza,Arusha

Tatizo la tapia mlo kwa watoto chini ya miaka mitano na wanawake walio kwenye umri wa kuzaa limepata ufumbuzi baada ya baada ya taasisi ya utafiti ya selian ilipo mkoani Arusha kuja na suluhisho la maharage bora yenye wezo wa kupunguza tatizo hilo

 

Akiongea na waandishi wa habari wa kanda ya kaskazini wakati wa ziara ya kimafunzo ilioandaliwa Tume ya taifa ya sayansi Teknolojia na ubunifu (COSTECH) mtafiti kutoka kituo cha utafiti cha Selian(SARI) kilichopo jijini Arusha Shida Nestory Mahenge  alisema kuwa tatizo la watoto na wanawake walio katika umri wa kuzaa ndio ulikuwa chachu ya upatikanaji wa mbegu za maharage haya ambayo yana madini ya chuma pamoja na zinki

 

Maharage haya yenye madini  ya chuma na zinki yanazalishwa katika hali ya kawaida ya kiagronomia aina hizi za maarage ya chuma na zinki ni haya tuliyoyataja ya Selian14 pamoja na selian15 na maharage haya ni mazuri kwani madini ya chuma na zinki ni muhimu sana katika mwili wa binadamu

 

Alibainisha maharage haya yanamadini ya chuma ambayo yanasaidia kuongeza chembechembe nyekundu  za damu ambazo  ni muhimu sana kwenye kusafirisha hewa ya oksijeni kwa ajili ya uhai  hivyo ni muhimu jamii ikiajijengea tabia ya kutumia maharage haya

 

Mtafiti huyo alienda mbali na kusema kuwa Tanzania  iliweza kupitisha aina mbili   za mbegu bora zenye madini ya chuma na zinki kwa wingi ambazo alizitaja mbegu hizo kuwa ni Selian14 pamoja na Selian 15 .

 

Alibainisha kuwa Takwimu za afya na viashiria vya malaria iliyofanywa mwaka  2015-2016inaonyesha kuwa upungufu wa samu kwa watoto wenye umri wa kati ya miezi sita -59ni kwa asilimia 58 ambapo asilimia 26wanaupungufu wa damu wakawaida na asilimia 30 wanaupungufu wa damu wa kati huku asilimia mbili wanaupungufu wa damu wa juu.

 

Alifafanua kuwa asilimia 45 ya wanawake wa Tannzania walio katika umri wa uzazi kuanzia miaka 15 hadi miaka 49 baadhi yao wanakabiliwa na tatizo hilo la upungufu wa damu ambapo kati yao asilimia 33wanaupungufu wa damu wa kawaida na asilimi 11 wanaupungufu wa damu wa kati na asilimia moja wanaupungufu wa damu kwa kiwango kikubwa zaidi ,alibainisha kuwa  asilimia 70 ya vifo vinavyosababishwa na upungufu wa damu hutokea katika nchi za afrika

 

Aidha mathara mengine yanayosababishwa na upungufu wa madini ya chuma ni pamoja na mwili kuchoka mara mawazo  ,hivyo kutokana na takwimu hizi na tatizo hio kubwa la kiafya na kilishe waliona jamii inaitaji ufumbuzi wa  lishe kwa haraka hivyo wakaona nivyema watafute ufumbuzi huo na ndio wakaja na aina hizi mbili za maharage

 

Sifa ya maharage ya seliani 14 yanakiwango cha madini ya zinki 26.38kwa 41.65ppm nakiwango cha madini ya chuma 75.17-8535ppm muda wa kuyapika ni kuanzia dakika 19-40 pia yanaladha tamu na unaweza kupika kwa mchanganyiko wowote na hayaaribiki ladha

 

 

Sifa ya maharage ya selian15  kiwango chake cha madini ya chuma ni 74.22-8135ppm yanakiwango cha madini ya zinki 27.38-42.55ppm yanapikwa kwa muda wa dakika 19-40.

 

Kutokana na sifa za maharage haya ni vyema wananchi wakajitaidi kuyatumia katika milo yao hususa ni wale wanaotarajiwa kubeba ujauzito na hata  kwa watoto ambao wanatatizo la kupungukiwa damu.

 

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates