Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi, Noar Lembris ameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika kutekeleza mauaji ya kikatili ya marehemu Steven Jimmy (43)aliyeuawa kwa kipigo nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite,Pendael Mollel.
Rai hiyo ameitoa mapema katika ibada ya mazishi ya marehemu iliyofanyika nyumbani kwake katika kitongoji cha ilkiushin wilayani Arumeru na kuhudhuliwa na mamia ya waombolezaji waliofurika katika mazishi hayo huku wakiangua kilio na masikitiko
"Hili tukio ni baya sana ninachotaka wahusika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria na wasirudi uraiani tena"alisema
Noar alisisitiza kuwa tukio hilo nila kinyama halipaswi kufumbiwa macho kwani binadamu hana wajibu wa kujichukulia sheria mkononi wakati vyombo vyenye dhamana ya kusimamia sheria vipo.
Aliwataka wananchi kulaani tukio hilo akisisitiza kuwa atalisimamia jambo hilo kwa ukamilifu na ikiwezekana wahusika wasirudi uraiani na waadhibiwe kwa mujibu wa sheria kwa matendo yao.
"Leo tunamzika mwenzetu aliyeuawa kikatili tukio hili tunaoaswa kulilaani ili lisijirudie ,kwani binadamu tumekuwa wanyama tukithamini mali kuliko chochote lakini lazima tutambue juwa mali inatafutwa lakini uhai haununuliwe popote"alisema
Mbunge huyo alitahadhalisha ndugu wa marehemu kutofanya chokochoko dhidi ya mjane kutaka mali za marehemu kama tabia ya watu wa kabila a kimasai wanavyofanya ,alisema atakuwa mstari wa mbele kupinga manyanyaso dhidi ya mjane ambaye ameachwa na marehemu akiwa na watoto watano wadogo na ujauzito wa miezi tisa.
Awali mchungaji Pius Steven wa kanisa Naioth Gosper Assembly aliwataka wananchi kutofanya malipizi juu ya tukio hilo ila kukataa roho za kuonewa kwa sababu damu inayomwagika bila sababu inamanung'uniko .
Alisema Marehemu Jimmy(43) amemaliza mwendo na maumivu aliyoyapata hatasikia tena,na waombolezaji wote hapa hakuna aliyesikia maumivu kama aliyoyasikia Steven.
"Haya yaliyotokea kwa mwenzetu Steven ni mjinga mmoja ndio ametekeleza unyama huu lazima atambue kuwa hata kama ni tajiri kiasi gani hata kuwa juu ya sheria, tuviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake"alisema.
Naye Mke wa marehemu, Joyce Ndanasila aliiomba serikali imsaidie kuwasomesha watoto wake watano ambao bado ni wadogo kwani hana msaasa wowote kwa sasa na nguzo yake kuu ilikuwa ni marehemu mumewe.
Marehemu Steven aliuawa kwa kipigo April 18 mwaka huu katika nyumba ya mfanyabiashara Pendael Mollel baada ya kutuhumiwa kuiba Pampu ya maji na ameacha mke mwenye ujauzito wa miezi tisa na watoto watano wadogo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia