KAMATI ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imeridhishwa na utendaji wa kazi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) baada ya kukagua ujenzi wa barabara ambazo wanazisimamia katika manispaa ya Iringa.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa TARURA wamekuwa wakifanya kazi nzuri za kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara kulingana na thamani ya fedha ambazo zimetolewa na serikali.
Moyo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Mtwira Darajani Ikonongo ya kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami kutasaidia kuchochea uchumi wa wananchi kwa kufanya shughuli zao kwa haraka Zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.
Alisema kuwa wilaya ya Iringa inamtandao wa barabara zinazotambulika zenye jumla ya kilometa 2173.44 ikiwa kilometa 1631.67 katika halmashauri ya wilaya ya Iringa na kilometa 541.77zipo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zote zipo chini ya TARURA.
Moyo alisema kuwa barabra hizo zote zinahudumia wananchi wa maeneo mbalimbali katika usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za uchumi ambazo zote hizo husaidia kukuza maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Iringa kwa ujumla.
Alisema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa imeridhishwa na utekelezwaji wa ujenzi wa barabara zilizopo chini ya TARURA na kuwata wataalam kuendelea kuwasimamia hivyo hivyo wakandarasi ambao wamepewa tenda ili watekeleze ujenzi kulingana na thamani ya fedha ambayo inakuwa imetolewa.
Wakati wa ziara hiyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ilimpongeza meneja wa TARURA wilaya ya Iringa Eng Barnabas Jabiry kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia vilivyo miradi ya ujenzi wa barabara ambazo wanazisimamia katika wilaya ya Iringa.
Awali meneja wa TARURA wilaya ya Iringa Eng Barnabas Jabiry alisema kuwa ujenzi wa barabra ya Mtwira Darajani Ikonongo ya kilometa 1.3 kwa kiwango cha lami utagharimu kiasi cha shilingi 500,000,000 hadi kukamilika.
Eng Jabiry alisema kuwa mradi huo ukikamilika utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa kata za Mkwawa,Mtwivila na Kihesa kwa kuwa itakuwa inapitia vizuri bila usumbufu wowote ule na kuwasaidia wananchi kufanya shughuli za uchumi bila usumbufu wowote ule.
Alisema kuwa mradi huoumeweza kutoa ajira 76 kati ya hao wanawake 10 wanaume 66 ambao wote wanapatikana katika kata hiyo na maeneo ambayo yanaizunguka kata hiyo
Eng Jabiry alisema kuwa anaishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha ukarabati za vijijini na mjini pamoja na madaraja ili kurahisisha usafiri nauchukuzi kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabra kutoka shilingi bilioni 1.46 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kufikia shilingi bilioni 2.46 kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia Zaidi ya 68.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia