Mhandisi Profesa Fredrick Kahimba akiongea na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya mafunzo ya kuandika habari za sayansi na teknnolojia yalioandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) (habari na picha na Woinde Shizza ).
Wakulima
wadogo na binafsi wa miwa nchini wanatarajia kuondokana na
changamoto ya kukosa masoko ya bidhaa zao baada ya taasisi ya Uhandisi na
Usanifu Mitambo nchini (Temdo) kutengeneza mitambo midogo yenye uwezo wa
kuzalisha tani moja hadi 10 za sukari kwa saa moja.
Akizungumza jijini Arusha katika mafunzo kwa Waandishi wa
Habari kutoka Kanda ya Kaskazini na yaliyoratibiwa na tume ya taifa ya Sayansi
Teknolojia na Ubunifuni (COSTECH), mkurugenzi mkuu wa TEMDO Mhandisi Fredrick Kahimba alisema kuwa kukamilika kwa
mashine hii kutamrahisishia sana mkulima kuzalisha sukari kiurahisi
Alisema kuwa mara nyingi viwanda huwa vinavuna kwanza
miwa yao kisha uangalia iwapo wanahitaji miwa zaidi kutoka kwa wakulima binafsi
ambayo mara nyingi ni sehemu ndogo tu hivyo wakulima wengi wamekua wakikosa
soko.
“Katika kipindi cha mwaka
2021/2022 tutakua tumetengeneza mashine mbili za mfano ambazo tutazipeleka kwa
wakulima ambao watatupa mapendekezo ya mwisho ambayo tutayazingatia kwenye
utengenezaji wa mashine na zaidi pia tunatarajia
hadi kufikia mwezi april tutakuwa tumemaliza mashine moja ,” amesema Profesa
Kahimba
Amesema utengenezaji wa
mashine hizo utakua mkombozi kwa wakulima wa miwa nchini ambao wataondokana na
utegemezi wa kuuza miwa yao viwandani na kuanza kuchakata miwa yao kwaajili ya
kuzalisha sukari ambayo kwa nyakati tofauti nchi imekua ikipata upungufu.
Akizungumza jijini Arusha katika
mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka Kanda ya Kaskazini na yaliyoratibiwa na
tume ya taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifuni (COSTECH), Mkuu wa Kitengo cha
mawasiliano na masoko kutoka TEMDO, Dk. Sigisbert Mmasi alisema kuwa TEMDO kwa zaidi ya miaka 30 wametengeneza
mashine za aina mbalimbali za kilimo, viwandani pamoja na kutoa elimu kwa
wahandisi na mafundi uchundo nchini.