mkuu wa wilaya ya Arumeru Muhandisi Richard Ruyango katikati akikata utepe ishara ya kufungua rasmi tawi la benki ya CRDB la Meru lililokuwa limefugwa Kwa ajili ya maboresho kushoto ni afisa mkuu uendeshaji wa benki ya CRDB Bruce Mwile
mkuu wa wilaya ya Arumeru Muhandisi Richard Ruyango wa nne kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani pamoja na mameneja wa benki ya CRDB mkoa wa Arusha mara baada ya kufungua Tawi jipya la benki hiyo lilikuwa limefugwa Kwa ajili ya maboresho lilijulikana Kwa jina la Meru brand
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Taasisi za kibenki ikiwemo benki ya CRDB zimetakiwa kuwapa wateja na wananchi wote kwa ujumla elimu juu ya umuhimu wa kuweka akiba, kukopa , kurejesha na kufanya shughuli za malipo kupitia benki ili waweze kukuza uchumi wao , kulinda fedha zao pamoja na kukuza mitaji yao.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Muhandisi Richard Ruyango alipokuwa akisoma risala ya ufunguzi wa tawi la benki ya CRDB Meru lilikuwa limefugwa Kwa ajili ya maboresho lililopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela juzi ambapo alisema iwapo watafanya hivyo watasaidia serikali kujua mapato halisi ya kila mtanzania na hata katika ukusanyaji wa kodi
Aidha pia aliwataka kuwaelimishwa wananchi kwamba, wakiwa na akaunti benki, pesa zao zitakuwa salama na wakifanya malipo kupitia benki wanatajijengea historia nzuri ya kukopesheka.
Aliwataka benki hiyo kuendelea kubuni mipango mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia benki,ambapo alitoa wito kwa watanzania wote kujenga mazoea ya kuweka akiba zao benki na kutumia benki kwa shughuli zao halali za kifedha.
Aidha pia aliitaka taasisi hiyo ya kibenki kulegeza masharti na vigezo vya upatikanaji wa mikopo ili kuweza kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi ,ambapo alifafanua kuwa anatambua katika eneo la riba wamefanya maboresho makubwa sana hususani katika sekta ya kilimo ambapo riba imeshushwa hadi asilimia 9, vivyo hivyo aliwataka wakaboreshe katika vigezo ili kuvutia wajasiriamali wengi kujitokeza.
"naomba niwakumbushe Wananchi wanachukuwa mikopo kwamba mikopo itolewayo na benki ni lazima itumike kwa uadilifu ili iweze kuwa na tija na mpate kurudisha na wengine wakope, tukijenga uaminifu huu ni imani yangu tutakuwa tukikopesheka zaidi"alifafanua Ruyango
Kwa upande wake afisa mkuu uendeshaji wa benki ya CRDB Bruce Mwile alisema kuwa hapo awali benki hiyo kupitia tawi la Meru limekuwa likitoa huduma za kawaida Kwa wateja wote lakini Kwa sasa kutokana na kuongezeka mahitaji ya wateja waliona umuhimu wa kuboresha huduma za tawi Ili kuendana na mahitaji yaliopo Sasa na baadae.
"Baada ya kufanya utafiti wa kina benki iliamua kufanya maboresho ya jengo Kwa kuongeza nafasi Kwa ajili ya kuhudumia wateja wengi zaidi pamoja na kuanzisha huduma Kwa wateja maalam(premier center)ambayo aikuwepo katika tawi hili awali pia tumeboresha huduma mbalimbali zilizokuwepo kama huduma ya utunzaji wa amana kupitia akaunti mbalimbali"alisema Mwile
Alisema kuwa hivi karibuni benki hiyo imesaini mkataba wa makubaliano wa mikopo na dhamana ya mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 182 Kwa ajili ya kuwezesha benki kukopesha wajasiriamali ambao biashara zao ziliathiriwa na janga la UVIKO-19 hivyo hiyo ni fursa kubwa Kwa wateja hivyo wajitokeze Kwa wingi kuchangamkia fursa hii .
Alibainisha kuwa anaamini kuwa kupitia tawi hilo fedha hizo zitakwenda kusaidia kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya kutoa na kupokekelea huduma ,hii ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi katika mkoa wa Arusha Kwa kufungua fursa mpya za masuala ya fedha mikopo na uwekezaji.