BREAKING NEWS

Monday, April 25, 2022

KATIBU MKUU UVCCM AONYA RUSHWA UCHAGUZI WA CCM

 



Katibu mkuu wa umoja wa Vijana (UVCCM) taifa Kenani Kihongosi akiongea na vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi

Baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa wakimsikiliza katibu mkuu wa UVCCM taifa Kenani Kihongosi

Na Fredy Mgunda,Iringa.

KATIBU mkuu wa umoja wa Vijana (UVCCM) taifa Kenani Kihongosi amewataka vijana wa umoja huo kwenda kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kulingana na uwezo wako.

Kihongosi alisema kuwa katiba ya chama cha mapinduzi inamtaka mwanachama yeyote anahaki ya kugombea nafasi yoyote bila ya kuwa na uwoga wowote ule.

Akizungumza wakati wa kongamano maalum la umoja wa vijana mkoa wa Iringa(UVCCM) kuacha tabia ya kulalamika kuwa wananyimwa nafasi za uongozi lakini kipindi cha uchaguzi vijana hao hawajitokezi kugombea.

Kihongosi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawaamini vijana ndio maana kwenye teuzi mbalimbali za serikali,ameteua Zaidi ya asilimia 75 hadi themanini za vijana kwenye kuongoza serikali ya awamu ya sita.

Aliagiza kwa makatibu wote wa UVCCM Tanzania kuacha mara moja kuwabeba wagombea,waache wanachama waamue nani anastahili kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye anauwezo wa kuongoza jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.

Kihongosi alisema kuwa hataki kusikia fomu za wagombea zinapotelea ofisini bali fomu zote zinatakiwa kufika sehemu husika ili vikao husika viweze kutoa maamuzi kwa mjibu wa katiba ya chama.

Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu atasimamia kanuni na sheria za chama hicho ili kupata viongozi bora ambao wataweza kukiongoza chama hicho na wanachama chake kwa kuwa rushwa haina nafasi mwaka huu.

Aidha Kihongosi aliwataka vijana wa umoja huo kucha tabia ya kuwapiga majungu vijana wenzao ili kila mmoja apate nafasi anayostahili kulingana na nafasi anayoishika naanayoigombea.

“Ni marufuku kwa viongozi kupanga safu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa kufanya hivyo kutapekea chama kupata viongozi wabovu ambao hawastahili kuwa viongozi” alisema Kihongosi

Alisema kuwa mwaka huu ni mwaka wa zoezi la SENSA hivyo wananchi wote wanatakiwa kujitokeza,kuhimizana na kujitokeza kuhesabiwa wakati ukifika ili serikali iweze kujua namna ya kupanga bajeti na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Kihongosi alisema kuwa vijana wanawajibu wa kujitokeza kuhesabiwa na kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza kuhesabiwa wakati wa zoezi la SENSA.

Kwa upande wake Katibu wa ccm mkoa wa Iringa Rukia Mkindu amewataka vijana wa umoja wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa (UVCCM) kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kuanzia ngazi ya shina hadi taifa kwa lengo la kuongeza chama hicho.

Mkindu aliwaomba vijana hao kuwa wanapoenda kugombea kuacha tabia ya kupokea na kutoa rushwa kwa kufanya hivyo kutatoa viongozi ambao sio bora kukiongoza chama hicho hapo baadae.

Aidha katibu wa Iringa Mkindu alitumia muda huo kumpongeza katibu mkuu wa umoja wa vijana taifa Kenani Kihongosi kwa kuchaguliwa kuwa katibu mkuu na kufanya kazi kubwa katika umoja huo kwa muda mfupi alipochaguliwa kuwa kiongozi.

Mkindu alimazia kwa kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa.

Naye Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliwataka vijana wa chama cha mapinduzi kuendelea kuelezea mafanikio ya muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo serikali kwa kipindi chote ilivyofanya kazi kuleta maendeleo.

Moyo alisema kuwa vijana wanawajibu wa kuwapinga watu wote ambao wanampango wa kuuvunja muungano kwa nia ovu zao hivyo vijana ndio wanajukumu la kuulinda muungano.

Alisema kuwa vijana wanaoenda kugombea wanatakiwa kuwa wanaccm kweli na sio mamluki wanaopandikizwa kwa lengo la kuja kukivuruga chama hicho hivyo wanatakiwa kuwa makini kwenye chaguzi za chama.

Moyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Iringa hautakubari kuona wagombea wanashinda kwa kutoa rushwa hivyo TAKUKURU itakuwa macho muda wote.

Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi safi ambao watakiongoza chama hicho kwa mafanikio ya kukivusha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali ambazo chama hicho kitashiriki kutafuta mamlaka ya kuunda serikali.

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates