WATANZANIA WAASWA KUITUNZA NA KUOMBEA AMANI YA NCHI


 Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa   akizungumza na waandishi wa habari mara baada tu ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha


 Umati wa wakazi wa 
mkoa wa Arusha waliofurika katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Kilimanjaro(KIA) kumpokea Nabii B.G Malisa ambaye atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini A
rusha

Na Woinde Shizza,Arusha
 Watanzania wametakiwa kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kufanya matukio ambayo yanaweza kuchochea vurugu na hatari ya kuliingiza taifa katika hali ya machafuko. 


Wito huo umetolewa jana na mchungaji kiongozi wa kanisa la Ukombozi hapa nchini, Nabii B. G Malisa wakati alipokuwa akihubiri neno la Mungu katika viwanja vya reli jijini Arusha. 



Nabii Malisa alisema kwamba watanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanaombea amani ya nchi inaendelea kutawala hapa nchini.



Alisema ya kwamba amekuwa akifanya ziara mbalimbali katika nchi mbalimbali duniani na kushuhudia hali ya usalama ikiwa tete ambapo askari wamekuwa wakitembea mitaani huku wameshika silaha za moto. 



"Hivi karibuni nilikuwa Nigeria wakati nashuka uwanja wa ndege nilipokelewa na askari wenye silaha za moto nikajiuliza maswali mengi sana kuhusu amani tuliyonayo hapa Tanzania "alisema Malisa 



Hatahivyo, alitoa wito kwa serikali kuunga mkono juhudi za viongozi mbalimbali wa dini hapa nchini katika kuwasaidia vijana na kusema viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa katika kuwainua watu kiuchumi na kuwaepusha na vitendo viovu. 



Awali akizungumza na waandishi wa habari mchungaji wa kanisa la Ukombozi tawi la Arusha Mchungaji Ushindi alisema kwamba mhubiri huyo atakwenda kufanya huduma ya maombezi mkoani Arusha kwa siku nane na kuwataka wakazi hao kujitokeza kwa wingi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post