Ticker

6/recent/ticker-posts

MKUU WA WILAYA YA IRINGA AKUTANA NA WAENDESHA DALADALA






Na Mathias Canal

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekutana na umoja wa wamiliki wa Daladala Wilayani Iringa katika ukumbi wa Siasa na kilimo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Baadhi ya madereva na Makondakta wameomba kurudishwa katika Stendi ya miyomboni kama ilivyo kuwa hapo awali wakidai kuwa eneo la walilohamishiwa kwa sasa la Mashine tatu ni finyu na lina msongamano mkubwa wa watu jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wananchi.

Dc Kasesela amesema kuwa kurudi katika standi ya miyomboni ni jambo lisilo wezekana kutokana na eneo hilo kuwa dogo na limezungukwa na makazi ya watu pamoja na majengo makubwa ya biashara jambo ambalo linafanya eneo hilo kuwa hatarishi zaidi kama iwapo kunaweza kutokea janga la moto.

"Unajua Miyomboni ni padogo sana pia pamejibana sasa kama ikitokea moto umewaka pale ni ngumu sana kupafikia kwa wepesi lakini pia Watu wa zima moto ndio waliopendekeza kuwa kituo kile kihamishwe sasa nadhani mnafahamu kuwa sheria ya zimamoto huwa ni ngumu kuipinga" Alisema Kasesera

Lakini pia amewataka madereva kuacha kutumika kisiasa kwani wanaofanya hivo wanafanya kwa maslahi yao binafsi.

Post a Comment

0 Comments