Na Woinde Shizza Arusha.
kutengua hukumu ya Mahakama Kuu ya jaji Sivangirwa Mwangesi kwa kumtangaza Nangole kama mshindi halali wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Longido.
Aidha katika hoja zao sita walizowasilisha waliiomba Mahakama ya Rufaa kufuta hati iliyotolewa na Jaji Mwangesi ikimjulisha Mkurugenzi wa Uchaguzi kwamba matokeo ya Jimbo la Longido yalifutwa na Mahakama Kuu.
Mawakili hao waliiomba Mahakama ya Rufaa kuamuru kwamba Dk Kiruswa ambae ni mjibu maombi alipe gharama za kesi katika Mahakama Kuu na gharama za Rufaa hii.
Walidai kuwa Jaji Mwangesi alikosea kisheria kwa kushindwa kuamua iwapo kilichotokea kwenye chumba cha majumuisho ya kura ilikuwa vurugu au mzozo tu wa maneno.
Pia walidai Jaji alikosea kwa kutotamka kwamba Dk Kiruswa aliamua kuondoka kwenye chumba cha majumuisho ya kura kwa makusudi na utashi wake mwenyewe.
Hoja nyingine ni kwamba Jaji alikosea pale alipotamka kwamba mazingira ya chumba cha majumuisho ya kura yasingeruhusu majumuisho ya kura ambayo yanaendana na utashi wa wapiga kura katika jimbo la Longido.
Wamedai Jaji alipotoka kwa kusema kulikuwa na kasoro nyingine tano zilizosababisha Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo kutangaza matokeo bila ya kuwapo kwa Dk Kiruswa.
Na hoja ya sita ni walidai kwamba Jaji alikosea kisheria kwa
kutotambua ujanja wa Dk Kiruswa alipodai eti kwamba yeye na timu yake hawakuwahi kufanya majumuisho yao wenyewe ya kura alizopata kwa mujibu wa fomu 21B za vituo vyote 175 va Jimbo la Longido.
Awali , Dk Kiruswa kupitia kwa mawakili watatu Dk Masumbuko Lamwai aliyekuwa akisaidiwa na David Haraka na Edmund Ngemera, waliwasilisha rufaa kinzani (cross appeal) yenye sababu mbili ambazo hazikuzuia mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo.
Katika maamuzi yake mahakama hiyo chini ya jaji kiongozi wa
jopo la majaji watatuSauda Mjasiri alisema maamuzi yote kuhusiana na shauri hilo watayatoa
katika maamuzi yao ya mwisho ndani ya muda mfupi ambao umepangwa kusikilizwa
kwa mashauri yote ya rufaa.
Katika kujibu hoja za upande wa watuma maombi wakili Lamwai
aliomba mahakama kuukubali uamuzi uliotolewa na jaji mwangesi kwani ulizingatia
misingi yote ya kisheria.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hakukua na
shaka kuwa uchaguzi ulikiuka misingi yake na njia pekee ilikua ni kuufuta na
kurudia upya.