Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Mbunge wa vijana mkoa kigoma zainab Katimba amesema ili
vijana nchini waweze kubadili maisha yao, kujijenga kiuchumi, kielimu
na kujitegemea, hawana budi kuiga na kufuata nyayo za maisha aliyoishi
Baba wa Taifa marehemu Mwalimu julisu kanbarage Nyerere.
Amesema Mwalimu Nyerere katika maisha yake aliamini kazi
ndiyo heshima ya kila mtu, kazi humpa mtu heshima na kukuza thamani ya
utu wa mtu mahali na wakati wowote alipo .
Katimba alitoa matamshi hayo juzi wakati aliposhiriki
katika kongamano la kukumbuka siku ya kifo cha muasisi wa Taifa letu
Mwalimu Nyerere huko Kigoma Mjini Mkoani hapa.
Alisema kazi za uzalishajimali viwandani na mashambani
lazima zifanywe na vijana wenyewe kwasababu ndiyo nguvu kazi ya Taifa
pia kutokaana na uimara wa ujana walionao, upeo na ufahamu huwasaidia na
kuwafanya wabuni na kutenda kwa haraka na usahihi.
"Kufuata au kupita juu ya nyayo na kuiga maisha ya Mwalimu
Nyerere kijana anaweza kufaidika aidha katika kujijenga kiuchumi,
kisiasa na kiuongozi kwasabahu muasisi wetu aliishi kwa kimaadili,
kikazi na kinidhamu "alieleza Katimba.
Aidha aliwataka vijana mkoani kigoma kutambua na kufahamu
umuhimu wa dhana ya kujituma na kufanya kazi kwa bidii huku akieleza
kwamba changamoto zinazowakabili vijana mijini na vijijini atazifikisha
bungeni na serikali itazipatia ufumbuzi.
Pia aliwahimiza vijana wenzake wajenge utamaduni wa kupenda
kusoma vitabu vya historia, majarida na maandiko mbalimbali
yanayoelezea maisha ya Mwalimu Nyerere , alivyoanzisha chama TANU,
kupigania uhuru wa Tanganyika , kuanzishwa kwa Taifa la Tanzania na
kushiriki kwake harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.
"Mwalimu Nyerere katika maisha yake alipenda kujitolea kwa
hali na mali hakusubiri kutoa msaada wa aina yoyote aidha kwa kuombwa
au kwa masharti kwani alijiona ana haki na wajibu wa kumsaidia kila
binadamu na kumfanya awe huru "alieleza Mbunge huyo wa vijana
Hata hivyo aliipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais Dk John Magufuli kwa msisitizo wa kauli mbiu ya hapa kazi na
kusema kila mmoja ikiwa ataikubali kufanya kazi kwa bidii, Tanzania ya
maendeleo ya viwanda itawezekana, uchumi utaimarika na maisha bora
yatatimia.
Katimba aliwahimiza vijana kujikita katika kazi za kilimo,
ufugaji, uvuvi, kazi za mikono, ufundi pia za ujasiriamali na biashara
mbalimbali kwani alisema kijana kukaa bila kujituma hakuleti maana wala
utatuzi wa matatizo au changamoto zilizopo.
"Kila wakati ninapopata nafasi ya kuchangia au kupeleka
hoja binafsi bungeni nimekuwa niguswa na ugumu maisha ya vijana, huwa
sina mzaha, naibana serikali na kuitaka itoe majibu ya kuridhisha
"alieleza
Alisema kwasababu ameingia bungeni kwa minajili ya
kuwawakilisha vijana kamwe alusisitiza hataacha kutotetea au
kutopigania haki na maslahi yanayohusu maisha ya vijana kiuchumi,
kisiasa na kimaendeleo.