MAKADA WA CCM ARUSHA NUSURA WAZICHAPE WAGOMBEA ENEO

Na Woinde Shizza ,Arusha

Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kata ya Moshono na
Moivaro wamenusurika kuzichapa kavukavu wakigombea eneo huku kila upande ukidai
Eneo hilo ni mali yake halali.


Vurugu hizo ziliibuka jana kufuatia
baada ya baadhi ya makada wa kata ya Moivaro  pamoja na viongozi wao
kuandamana hadi ofisi za CCM kata ya Moshono
Kia madai eneo hilo ambako kumejengwa ofisi za Ccm ni mali yao halali.


Hali hiyo ilipelekea makada wa pande hizo mbili kurushiana maneno makali
nusura wazichape lakini baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya wilaya waliingilia
kati na kutuliza hali ya hewa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya makada wa CCM kata ya Moivaro
walisema kwamba eneo hilo ni mali yao halali tangu miaka ya nyuma na
kinachoendelea ni hujuma zinazofanywa na viongozi wa CCM kata ya Moshono kutaka
kulipora.


Michael Mnyaa pamoja na Swalehe Abadalla ambao ni makada wa CCM kata
ya Moivaro walisema kwamba
wanashangaa uongozi wa CCM kata ya Moshono kung”ang”ania eneo hilo kinyume na
sheria ihali sio mali yao.Wanachama hao walisema ya kwamba suala hilo
walishaliwasilisha mbele ya uongozi wa CCM ngazi ya wilaya na walipewa
majibu ya kwamba eneo hilo ni mali halali ya CCM kata ya Moivaro.



Hatahivyo,Rashid Kimario pamoja na Eliufoo Mollel walisema kwa nyakati
tofauti ya kwamba eneo hilo ni mali ya CCM kata ya Moshono tangu enzi za Tanu.


Absolom Loibon,ambaye ni kada wa CCM kata ya Moshono alisema kwamba
chanzo cha mgogoro huo ni kugawanywa kwa kata hizo mbili na kudai kwamba
wanaomba serikali irejeshe mipaka ya mtaa wa Kazkazini ili kutuliza hali ya
hewa.



Hatahivyo,katibu wa  CCM kata ya Moshono,Lucy
Siringo alisema kwamba wanashangaa makada wa CCM kutoka kata ya Moivaro kudai
eneo hilo ni mali yao ihali wao wamejenga ofisi ya chama katika eneo hilo.


“Hili eneo ni tawi halali la CCM kata ya Moshono tunawashangaa hawa
wenzetu kudai eneo hili ni mali yao”alisema Siringo


Hatahivyo,Siringo alidai ya kwamba wanahisi kuna njama zinazofanywa na
viongozi wa CCM ngazi ya kutaka kuwanyang”anya  eneo hilo na
kutahadharisha kuwa wako tayari
kurejesha kadi za CCM endapo mpango huo ukifanyika.


Katibu wa CCM wilaya ya Arusha,Ferooz Bano alipoulizwa kuhusu suala hilo
alisema kwamba wanautambua mgogoro huo nab ado unashughulikiwa katika ngazi ya
wilaya na kuzitaka pande hizo mbili kupunguza jazba.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post