Ticker

6/recent/ticker-posts

WALIMU KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akikabidhi Tuzo ya Mwalimu Bora
kwa Mwalimu Pili Omari Makota wa shule ya Msingi Uraki katikati ni
Mkurugenzi wa Shirika la The Foundation For Tomorrow Melissa Queyquep. Tuzo
za Walimu Bora ziliandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la The
Foundation For Tomorrow  jana jijini Arusha na kufanyika katika shule ya
msingi Arusha schoo
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akikabidhi Tuzo ya Mwalimu Bora
kwa Mwalimu Regina Lekule wa shule ya Msingi Msitu wa Mbogo, katikati ni
Mkurugenzi wa Shirika la The Foundation For Tomorrow Melissa Queyquep. Tuzo
za Walimu Bora ziliandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la The
Foundation For Tomorrow  jana jijini Arusha na kufanyika katika shule ya
msingi Arusha school

 Na Woinde Shizza,Arusha
 Walimu nchini wametakiwa kuhamasisha Wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi
hasa katika kipindi hiki ambacho taifa  linaelekea kwenye uchumi wa viwanda
ili kuweza kupata wataalamu wa kutosha.



Akizungumza katika Utoaji wa Tuzo kwa walimu bora  katika wilaya ya Arusha
mjini na Arumeru ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro  amewataka
Walimu nchini kuwa wabunifu na kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya
sayansi ambayo ni chachu ya maendeleo ya nchi.



Alisema kuwa serikali inatambua kuwa Walimu ni Injini ya elimu bila walimu
elimu haiwezi kusonga mbele hivyo walimu watumie nafasi zao katika
kuhakikisha kuwa serikali inavuna wataalamu waliobobea katika masomo ya
sayansi kwa kuwajengea misingi bora.



“Hatuwezi kupata Wataalamu wa kutosha viwandani kama hatutahamasisha masomo
ya sayansi mashuleni nchi itakuwa na utegemezi mkubwa wataalamu kutoka nje
ya nchi” Alisema Mkuu wa Wilaya



Mkurugenzi wa Shirika la The Foundation For Tomorrow Melissa Queyquep ambao
ni waandaaji wa tuzo hizo alisema kuwa Tuzo hizo zimetolewa kwa walimu kwa
kutambua mchango wa Walimu katika kuhakikisha kuwa Watoto wanapata elimu
bora itakayowakomboa kifikra,kijamii na kiuchumi.



“Tumezingatia vigezo vingi katika utoaji wa tuzo hizi ikiwemo uwezo wa
kuchochea ufikiri na uchambuzi kwa watoto,Ubunifu na uvumbuzi,Anafundisha
kwa mifano zaidi kuliko maelezo,uwezo wa kushawishi na kuhamasisha
wanafunzi kujifunza,haiba pamoja na uzoefu kazini” Alisema Melisa


Jumla ya Walimu 10 wamepata tuzo za Walimu bora kutoka Wilaya ya Arusha
mjini na Wilaya ya Arumeru,Baadhi ya Walimu hao ni Regina Lekule,Ally
Msongo,Pili Mokoka,Evelina Sanga,Neema Lema,Swahibu Issa,Nicholous
Michael,Frida Malia,Asumpta Mbuda na Paulina Lolo.

Post a Comment

0 Comments