VIONGOZI UWT CCM TAIFA WAKUMBUSHA UTEKELEZAJI WA ILANI CCM RUKWA.


MJUMBE wa Halmashauri kuu CCM Taifa Nadra Rashid amesema amani,umoja na mshikamano ndiyo msingi wa maendeleo katika nchi na kuwataka wanawake wa UWT CCM mkoa wa Rukwa kuwalea vijana katika maadili mema ili kupata kizazi chenye utu na mshikamano ndani ya Taifa.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa Nadra Rashid akiwa ameambatana na Beng'i Issa Mbunge viti maalum kundi la wafanyakazi, amesema lengo la ziara hiyo ni kukumbushana na kuhimizan utekelezaji wa ilani katika miradi ya maendeleo ya 2025/20230, ikiwemo miradi ya vikundi vya asilimia 10 na kuwapongeza wanachama kwa kukichagua chama hicho kuendelea kuongoza nchi.

Amesema " mwanamke ndiye mlezi wa famili katika ngazi ya Familia na jamii na kwamba maadili katika familia yanaanzia kwa mwanamke,tuwalee vijana wetu katika msingi wa maadili ya Kitanzania".

Pia amewataka vingozi wa jumuiya ya wanawake CCM kuendelea kuhubiri amani,umoja na mshikamano ambao ni msingi wa maendeleo ndani ya chama na nchi kwa ujumla.

Aidha amewapongeza wanawake waliothubutu kuchukua mikopo ya asilimia 10, na kuwa malengo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwainua wanawake kiuchumi.

Kwa upande wake katibu wa UWT CCM mkoa wa Rukwa Aligila Salinyambo amewashukuru viongozi hao na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa chama na serikali ili kudumisha umoja na ushirikiano ndani ya chama na serikali.

WABUNGE viti maalum kutoka makundi ya wafanyakazi, vyuo na vyuo vikuu, wakiongozwa na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT CCM Taifa Hawa Ghasia wamewasili mkoani Rukwa kwa ziara ya siku tatu kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo ya Chama na serikali ya utekelezaji wa ilani ya 2025/2030 ya chama hicho.












About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia