Bolt Yawezesha Watumiaji Kuomba Safari Kupitia ChatGPT Nchini Tanzania

 




Mwandishi wetu, DSM



Bolt imewezesha huduma zake za usafiri wa mtandao kupatikana kupitia ChatGPT nchini Tanzania, kufuatia ujumuishaji wa kimataifa ulioanza kutekelezwa katika masoko yote ambako kampuni hiyo inafanya kazi.


Hatua hiyo inaashiria mabadiliko makubwa katika namna wananchi wanavyofikia huduma za usafiri. 


Kwa miaka mingi, kuomba safari kulihitaji mtumiaji kufungua programu maalumu ya usafiri wa mtandao na wakati mwingine kusubiri ipakie.



Kwa mujibu wa Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole Alisema kuwa mpango huo utaleta mapinduzi makubwa sana.



Aidha kwa  Sasa, mtumiaji anaweza kuanzisha mchakato huo ndani ya ChatGPT kwa kuuliza kuhusu safari, kuona makadirio ya awali ya nauli, kulinganisha njia mbalimbali na kubaini eneo linalofaa zaidi la kupandia, 


 Pia alisema kuwa kabla ya kukamilisha ombi kupitia programu ya Bolt.Kwa Tanzania, hatua hii itaaakisi mabadiliko mapana katika tabia za matumizi ya teknolojia. 


"ChatGPT na zana nyingine za Akili Mnemba (AI) zinazidi kuwa sehemu ya kazi, elimu, upangaji wa biashara na ufanyaji wa maamuzi miongoni mwa vijana, wataalamu, wajasiriamali na wanafunzi. "Aliongeza


Katika hatua nyingine alidai  kuwa programu ndani ya ChatGPT zimeundwa kuingia kwa urahisi katika mazungumzo, hivyo kuwawezesha watumiaji kuwasiliana na huduma za nje bila kuondoka katika mazingira ya mazungumzo.


“Ujumuishaji huu una maana kwamba huduma za usafiri sasa zinaingia katika mazingira yale yale ya kidijitali ambamo watu tayari hupanga shughuli zao, hufanya kazi, hujifunza na kufanya maamuzi,” Kanyankole.


 Kanyankole alisema kuwa pia programu hiyo inauwezo wa kuomba safari ya Bolt kutoka katika mazingira hayo hayo na inaweza  u

Kupunguza hatua zisizo za lazima na kufanya upangaji wa safari kuwa rahisi, wa haraka na wenye mtiririko mzuri zaidi,”


 Aliongeza Ubunifu huo unakuja wakati Akili Mnemba ikizidi kubadili mwenendo wa usafiri duniani. Utafiti wa Accenture Consumer Pulse Research 2025, uliowahusisha watumiaji 18,000 katika nchi 14, unaonesha kuwa asilimia 80 ya wasafiri katika sampuli hiyo hutumia zana za Akili Mnemba zalishi kwa madhumuni yanayohusiana na usafiri.Nchini Tanzania, manufaa yanaweza kuonekana moja kwa moja kupitia upangaji wa haraka wa safari kwa wafanyakazi wa ofisini, maamuzi rahisi ya usafiri kwa wanafunzi, uelewa bora wa njia kwa wasafiri wa kikazi na uzoefu mwepesi zaidi kwa abiria wanaotegemea zana za kidijitali.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia