WAFUGAJI WAHAMASISHWA KUTUMIA MBEGU BORA ZA MIFUGO KUONGEZA TIJA

Wafugaji  wametakiwa kufunga mifugo yenye ubora na kuaachana na ufugaji wa mifugo ambayo Haina ubora kwani Hali hiyo ya ufugaji wa mifugo yenye mbegu duni inasababisha washindwe kunufaika na ufugaji wao.


Hayo yameelezwa na meneja wa shamba la West Kilimanjaro  Ranchi, Adil  Butt, akiongea kwenye maonesho ya mifugo hususani  wa shamba Hilo la West Kilimanjaro katika viwanja vya maonesho ya nane nane  yanayoendelea Njiro Arusha


Amesema ushiriki wao katika maonyesho ya kilimo na mifugo unalenga kuhamasisha Watanzania kufuga mifugo yenye tija kwa kutumia mbegu bora zinazoweza kuongeza uzalishaji wa nyama na kuboresha kipato cha wafugaji.


 Adil alisema wamewasilisha mifugo ya aina mbalimbali ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo ili wananchi wajifunze kuhusu aina za mifugo inayofaa kwa mazingira ya Tanzania.


Alisema upande wa ng'ombe wameleta aina ya Boran, ambayo ni mbegu bora yenye asili ya Kenya na inayoweza kufikia uzito wa zaidi ya kilo 800, huku wakionyesha pia aina nyingine zinazofugwa katika shamba lao ikiwemo Simmental na Tuli.


Kwa upande wa kondoo, alisema wameleta aina za Meatmaster, Dorper, Red Maasai pamoja na Persian Blackhead kutoka Namibia ili kuongeza vinasaba vipya nchini na kuondoa changamoto ya kuzaliana kwa ukoo mmoja (inbreeding).


Adil alieleza kuwa baadhi ya mifugo hiyo imetoka Namibia na Afrika Kusini na imechaguliwa kutokana na uwezo wake wa kuhimili mazingira ya Tanzania, hususan maeneo yenye ukame.


Alisema katika kipindi cha miezi sita tangu waanze shughuli zao wameona mwitikio mkubwa kutoka kwa wafugaji wanaotembelea shamba lao, huku changamoto kubwa iliyobainika ikiwa ni upatikanaji wa malisho bora.

Aidha, 



Alifafanua kuwa  kampuni hiyo ipo eneo la Sanya, West Kilimanjaro, ambako imeanza shughuli zake rasmi mwaka 2024 kwa lengo la kusambaza mbegu bora za mifugo kwa wafugaji nchini.


Alibainisha kuwa wanatekeleza programu maalumu ya kuboresha vinasaba vya mifugo kwa kushirikiana na jamii, ambapo vikundi vya wafugaji vitasajiliwa na kupewa huduma za madume bora kwa ajili ya kuongeza ubora wa mifugo yao.


Pia alisema wanaendelea na ujenzi wa kituo cha kisasa cha uzalishaji wa mbegu na viinitete (Embryo and Semen Center), kitakachorahisisha usambazaji wa mbegu bora kwa wafugaji kupitia wataalamu wa mifugo.


Kwa mujibu wa Adil, kampuni hiyo inatumia zaidi ya hekta 2,500 za ardhi zilizotolewa kupitia NARCO kwa ajili ya kuendeleza shughuli za ufugaji wa kisasa na kuzalisha mifugo bora.


Aliongeza kuwa hadi sasa kampuni imeajiri wafanyakazi zaidi ya 210 kutoka kwenye jamii zinazozunguka eneo hilo, wakiwemo wanawake zaidi ya 50, jambo ambalo amesema linachangia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa wananchi wa maeneo husika.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia